Saturday, February 25, 2012

MUGABE NA URASI WA MAISHA.....


Kamati maalum ya katiba ya Zimbabwe imesema imerekebisha kipengele kimoja kwenye rasimu ya katiba ili Rais wa sasa Bw Robert Mugabe asiathiriwe katika uchaguzi ujao.

Kamati hiyo imesema imepitia na kurekebisha kipengele hicho ambacho kilileta malumbano baada ya baadhi ya vyombo vya habari kutoa habari zisizo sahihi kuhusu uwezekano wa Rais Mugabe kugombea urais katika uchaguzi unaokuja.

Mwenyekiti mwenza wa kamati hiyo Bw Munyaradzi Paul Mangwana amesema wamepitia ibara ya tano na ya sita ya rasimu ya katiba na kurekebisha kipengele kinachosema mgombea urais anatakiwa kuwa na umri wa miaka 40, raia wa Zimbabwe na ataongoza kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano.

No comments: