Saturday, February 25, 2012

UCHAGUZI MKUU SENEGAL NI KESHO... RAIS WADE atoa wito kwa raia

RAIS WADE

Raisi wa Senegali Abdoulaye Wade ametamatisha kampeni zake za uchaguzi kwa kuwashawishi raia kupuuzia madai ya upinzani ambayo yanapinga kiongozi huyo kugombea kwa awamu nyingine.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 85 alihutubia siku ya ijumaa ambapo umati wa watu huko Dakar ulijitokeza katika mbio za siku ya mwisho ya kampeni tayari kuelekea katika siku ya kupiga kura kesho jumapili.

No comments: