Thursday, July 21, 2011

MTWARA

Maandalizi ya maadhimisho ya siku ya mashujaa yamekamilika katika makaburi ya mashujaa Naliendele mkoani Mtwara, ambako shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika kitaifa july 25 mwaka huu.

Mnadhimu mkuu wa majeshi Luteni Generali Abdulrahman Amir Shimbo, amebainisha hay leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maandalizi ya shughuli hizo.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari Luten Generali Shimbo maadhimisho hayo yanafanyika tarehe 25 july kila mwaka amabayo ni kumbukumbu ya kurejea mashujaa waliotoka katika vita vya kagera.

Amesema hapo awali maadhimisho hayo yalikuwa yakifanyika mnamo tarehe 1 septemba , ikiwa ni siku ambayo iliasisiwa na wakoloni wa kiingereza kuwaenzio mashujaa waliop[igana katika vita vya pili vya dunia.

Amesema serikali iliona haja ya kuifanya siku hiyo kuwa ya kitaifa kwa kuwakumbuka mashujaa wote walioipigania nchi yetu pamoja na wale walioshiriki katika vita vya ukombozi katika nchi za jirani ikiwemo msumbiji.

katika hatua nyingine Luteni jeneraqli Shimbo amewataka wananchi wanaoishi maeneo ya jirani kutokushtuka, pale watakaposikia milio ya risasi ama milipuko kadhaa ya mizinga siku ya jumamosi ya tarehe 23, ambapo wanajeshi watakuwa wakifanya maandalio ya mwisho kwa ajili ya shughuli hiyo

Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika katika makaburi ya mashujaa naliendele mkoani hapa, huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Amir jesh mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama , Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kiwete.

Wengine wanaotarajiwa kuhudhuria ni waziri mkuu Mizengo Pinda , Rais wa Zanzibar , Dkt Ali Mohamed Shein, makamu wa pili wa rais Balozi Seifu Ali Iddi, marais wastaafu, pamoja na waambata wa kijeshi kutoka nchi jirani.


KUHAMISHWA MAKABURI HAYO KUTOKA MSUMBIJI.

Kwa mujibu wa Luteni jenerali Shimbo, Mnadhimu mkuu wa jeshi,

Makaburi hayo yalibidi kuhamishiwa mtwara kufuata haja ya ndugu za mashujaa waliofia msumbiji kutaka kuyaona makaburi ya ndugu zao.

Mwanzoni ililazimu watu hao wapelekwe Msumbiji kwa ajili ya kwenda kuona makaburi ya ndugu zao , lakini serikali ikaona ni vyema ikayahamishia makaburi hayo mkoani Mtwara eneo ambalo linapakana na msumbiji, eneo ambalo pia lilitumika sana kama njia kuu ya kuendea huko.

Hii leo eneo hilo lina makaburi 101, mashujaa hao wamelala hapo.

No comments: