Sunday, July 17, 2011

MTWARA

Siku mbili baada ya naibu waziri wa afya kuwataka wanaume kuhudhuria kliniki kwa ajili ya kupima afya zao, wakazi manispaa ya mtwara mikandani wamekuwa na maoni tofauti.

Wakizungumza na Info radio mapema leo wakazi hao wamesema kuwa suala la wanaume kuhudhuria kiliniki hususani kwa vijana litakuwa si jambo rahisi kutokana na kuona aibu kuhudhuria maeneo hayo.

Mmoja wa wananchi hao Bw,Boniface amesema kuwa ushauri huo sio mbaya na haoni mantiki yoyote ya vijana kusita kwenda kliniki kwani suala la afya sio suala la kuonea aibu na hasa kwa kuzingatia tatizo linalozungumziwa ni kansa.

Katika hatua nyingine wananchi hao wameshauri serikali kutoa elimu juu ya dalili na visababishi vya ugonjwa huo, ili kuweza kuwapa nafasi nzuri kuweza kujitathmini hali ya afya zao kila wakati.

Mapema ijumaa iliyopita bungeni mjini Dodoma , wakati akijibu swali la nyongeza Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya alishauri kuwa ni vyema wanaume wakajenga utaratibu wakwenda kliniki kufatia wengi wao kukumbwa na saratani ya kibofu.

DODOMA

Siku mbili baada ya bajeti ya wizara ya nishati na madini kuwasilishwa bungeni , imeelezwa kuwa bwawa la Mtera halitosimamishwa kuzalisha umeme kutokana na kupungua kwa kina cha maji kilichosababishwa na ukosefu wa mvu za kutosha.Mhandisi Mkuu wa Uendeshaji wa kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera ,Julius Chomolla amewaambia waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho kuwa kwa sasa wanazalisha umeme kwa masaa katika bwawa hilo ili uzalishaji usisimame kama ilivyotokea mwaka 2006.
Amesema kiwango kinachohitajika kuzalisha umeme ni mita 698.50 na cha chini mita 690 toka usawa wa bahari , ambapo hadi kufikia july 15 kilikuwa mita 690.74 , na kuongeza kuwa kituo hicho kinategemea miwili ambayo ni Ruaha Mkubwa na Ruaha na Mdogo na Kisigo wakati wa kipindi cha masika pekee.Kwa mujibu wa meneja huyo kiwango cha umeme kinachozalishwa kwa sasa hadi july 15 mwaka huu katika bwawa hilo ni Mega wati 33 badala ya Mega Wati 80, ikiwa ni pungufu ya megawati 47 uzalishaji unapokuwa katika hali ya kawaida.Wakati hali ikiwa hivyo huko mtera Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) ,Badra Masoud, anasema Vituo vingine vinvyozalisha umeme ni Kihansi kwa sasa ni Mega Wati 90 badala ya Mega Wati 180,Kidatu Mega Wati 40 badala ya 204, New Pangani Mega Wati 20 badala ya Mega Wati 168 na Nyumba ya Mungu ni MW3.5 badala ya MW 8.

KILIMANJARO

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa
(TAKUKURU) mkoani Kilimanjaro inatarajia kuingiza somo la Rushwa kwenye mitaala ya shule za Sekondari kwa ajili ya kuijengea jamii mazingira ya kuichukia rushwa tangu wakiwa wadogo. Hayo yamebainishwa na mkuu wa taasisi hiyo Bw,Lawrence Swema katika mafunzo yaliyohusisha walimu wa shule za Sekondari yaliyofanyika katika hotel ya YMCA Mjini Moshi. Swema amesema mafunzo hayo kwa waalimu yamefanyika kwa lengo la kupata maoni ya waalimu ambao wanafundisha somo la uraia jinsi ya kuingiza kipindi kinachohusiana na mambo ya rushwa kimtaala katika shule za sekondari. Amesema kuwa mchakato wa kuanzisha somo la rushwa mashuleni tayari umekwisha fanikiwa kwa kidato cha 5, huku mchakato ukiwa unaendelea kwa kidato cha 4 kwa kuwawezesha watu watakaousimamia mtaala huo. Katika hatua nyingine Bw Swema , amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la watumishi wengi kutumia vyeti vya bandia na vya watu wengine, hali ambayo inahusishwa na vitendo vya rushwa.

No comments: