Sunday, July 10, 2011

HABRI ZA KITAIFA ZA INFO RADIO JULY 10 , 2011

Na Elia Migongo

KILIMANJARO

Mkazi wa Kijiji cha Kware Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro Mustafa Elly (55)anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumpiga mke wake na kumsababishia kifo.
Wakizungumza na waandishi wa habari , Majirani wa mtuhumiwa ambao hawakutaka majina yao yatajwe wamesema kuwa marehemu alikuwa amepigwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili.
Kwa mujibu wa majirani hao familia hiyo ilikuwepo na ugomvi wa mara kwa mara,ambapo mtuhumiwa anadaiwa kumpiga mke wake Fatuma Musa (51) na kumpiga sehemu za miguuni mikono na kichwani bila kupeleka hospitali.
Mnamo julai 7 mtuhumiwa huyo alitaka kufanya mazishi ya mke wake julai 8 ambapo aliwashirikisha majirani na wakiwa katika hatua ya kuosha mwili wa mama huyo waligundua kuwa ana majereha sehemu mbalimbali za mwili na kutoa taarifa polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Hapa Absolom Mwakyoma amekiri kutokea kwa tukio , na kusema kuwa polisi inamshikilia mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakopokamilika.

DAR ES SALAAM

Muda mchache baada ya Sudani kusini kuwa taifa huru, Rais Jakaya Mrisho kikwete ametuma salamu za pongezi kwa kiongozi wa taifa hilo jipya ulimwenguni.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na ikulu ya Dar es salaam rais ametuma salamu hizo kwa niaba ya serikali yake na watanzania kwa ujumla.
Amesema kuwa wananchi wa tanzania wapo tayari kuanzisha uhusiano wa kidugu, kijamii , kiuchumi, na kidiplomasia wakati huu ambapo taifa hilo linakabiliwa na changamoto kadhaa.
Nchi ya Sudani kusini ilitangazwa rasmi kuwa taifa huru usiku wa kuamkia juma mosi, uamuzi ambao unafuatia maamuzi ya kura za maoni zilizopigwa na wannchi wa sehemu hiyo ya zamani ya taifa la Sudani.
Wadadisi wa mambo nchini wanasema taifa hilo la 54 barani afrika halina budi kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki wakati inatafuta kujiimarisha katika miundombinu, elimu , uchumi na afya.

MTWARA

Siku kumi baada ya mwaka wa fedha 2011/2012 kuanza, wakazi wa Mtwara wamelalamikia ongezeko kubwa la bei za mafuta ya taaa.
Wakizungumza na info radio kwa nyakati tofauti mapema leo, wananchi hao wamesema , hoja ya serikali kutaka kudhibiti uchakachuaji wa mafuta ya dizeli na petro kwa kupandisha bei ya mafuta ya taaa haikuwatazama wananchi wa hali ya chini.
Wamesema kupanda kwa bei ya ni shati hiyo ambayo imekuwa mkombozi kwa watanzania walio wengi kunapingana waziwazi na adhma ya serikali kuboresha maisha.
Wakazi hao wemesema haikuwa wakati muafaka kupandisha bei za nishati hiyo muhimu wakati huu ambapo huduma ya umeme haiwafkiii hata robo ya watanzania waishio vijijini.
Tangu july mosi pamekuwa na ongezeko la takribani shillingi 200 kwa kila lita moja ya mafuta ya taa na kufanya bei ya nishati hiyo kufikia shillingi 2000.

No comments: