Thursday, July 14, 2011

IGUNGA

Mbunge wa jimbo la igunga kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) bw, Rostam Azizi amejiuzulu nafasi hiyo pamoja na ile ya ujumbe wa kamati kuu.
Mbunge huyo ametangaza adhma ya kuachia nafasi hiyo wakati akizungumza na wazee wa jimboni kwake mjini igunga.
Amesema kwa kutambua kuwa uongozi ni dhamana’ dhana ambayo kila anapoitakari huwa inamrejesha nyuma na kukumbuka jinsi alivyoteliwa, miongoni mwa vijana wengi, kuwa mwakilishi wa Jimbo la Igunga tangu mwaka 1994.
Amesema ameamua kujiuzulu nafasi zake kwa kuanzia na ile ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Akiuwakilisha Mkoa wa Tabora na ile ya ubunge wa Igunga ambazo amesema bila baraka za chama chake Asingelikuwa nazo.
Amesema uamuzi wake unalengo la kuwajengea heshima na imani machoni mwa wanachama na wananchi wengine, viongozi wake ambao anaamini baada ya yeye kujitoa watapata fursa ya kutafakari upya changamoto nyingine mbadala zinazowakabili ambazo msingi wake ni dhamana kubwa walizo nazo za kukiongoza chama chama pamoja na serikali.
Amesema Uamuzi wake wa kuachia nafasi zake zote za uongozi alizopata kwa tiketi ya CCM haukutokana na wala haumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezaji wa dhana ya KUJIVUA GAMBA, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasa hizi uchwara na kutumia muda wangu kushughulika na biashara zake.
Kujiuzulu kwa Rostam kunafuatia Dhamira ya mwelekeo wa kufanya mabadiliko ya ndani ya chama iliYOtangazwa rasmi na Mwenyekiti , Rais Jakaya Kikwete wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, mjini Dodoma.


DODOMA

Wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa limepanga kutumia jumla ya shillingi billion 682, millioni 315, 415 elfu, ili kuweza kutekeleza majukumu mbalimbali katika mwaka wa fedha 2011/2012.
Hayo yamebainishwa na waziri wa wizara hiyo Bw, Hussein Mwinyi wakati akiwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake katika bajeti ya mwaka huu wa fedha.
Amesema kati ya fedha hizo shilling 533 billioni , 396 millioni, 593 elfu zitakuwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, huku 148 billioni , 918 millioni, 822 elfu kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Akitoa maoni ya kamati ya bunge inayoshughulikia mambo ya nje ,ulinzi na usalama, kwa niaba ya mwenyekiti wa kamati hiyo, amesema ili dhamira ya serikali ya kuboresha maslahi ya jeshi , mazingira yao ya kuishi ni vyema utekelezaji wa kulipa madeni binafsi ya wanajeshi ufanyike kwa wakati na kuharakisha zoezi la kurejesha zoezi la mafunzo ya JKT na kutenga fedha ya kutosha kwa ajili hiyo.
Naye waziri kivuli wa wizra hiyo Bw, Joseph Selasini amesema ni vyema jeshi likajizatiti katika uvumbuvi wa teknolojia ya vifaa kama magari pamoja na bunduki, ni vyema jeshi hilo likaanza kutumia vijana ambao watawalea na kuwafundisha kulingana na matakwa ya jeshi hilo.

MTWARA

Imeelezwa kuwa watu wengi mkoani Mtwara hawajui umuhimu wa kusajili , vizazi , vifo na ndoa kwa manufaa ya baadae.
Hayo yameelezwa leo na Bw,Nandule Saidi , wakati akizungumza na Info Radio ofisini kwake kwa niaba ya mkuu wa wilaya , ambapo amesema kuwa watu wengi hawajajisajili na kukimbilia kujisajili pindi panapoitajika vyeti vya kuzaliwa wakati kutafuta kazi
Amesema kuwa changamoto hiyo ya kutokujisajili imekuwa ikiwakabili zaidi watu wa vijijini huku wale wanaishi maeneo ya mijini wakijitokeza zaidi katika zoezi hilo mara tu wanapojifungua.
Aidha metanabaisha kuwa kwa kipindi cha January mpaka june mwaka huu kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaojisajili ambapo ambapo waliojisajili wanafikia 2,617.
Katika hatua nyingine Bw, Saidi ametoa wito kwa wananchi kwamba ni muhimu kuelewe kuwa usajili wa vizazi,vifo na ndoa ni muhimu kwa wazaliwa wa Mtwara na taifa kwa ujumla.

No comments: