Monday, May 2, 2011

MFAHAMU OSAMA BIN LADEN

MFAHAMU HAYATI OSAMA BIN LADEN

 Ni mtoto wa mjeni
 Aliishi maisha ya ufahari kabla ya kujitosa kwenye ugaidiOsama bin Laden alizawa mwaka wa 1957,
katika familia ya kitajiri nchini Saudi Arabia
Ana zaidi ya ndugu wa kiume na wa kike 50.

Baba yake Osama alimiliki kampuni kubwa ya ujenzi.
Mwanzoni mwa miaka ya themanini aliachana na mfumo wa maisha ya kifahari ambayo alilelewa, maisha haya ya starehe na kitajiri, akajiunga na vugu vugu la kupigania haki dhidi ya utawala wa kisovieti baada ya majeshi yake kuishambulia Afghanistan.

Na hapo akipigana pamoja na waarabu wenzake, ndipo alizindua kundi la kigaidi la Al qaeda.

Mnamo mwaka wa 1998, alitangaza FATWA yaani vita vikali vya kidini dhidi ya Marekani. Kufuatia ghadhabu aliyokuwa nayo na Marekani, kwa kuweka majeshi yake katika ardhi ya kiislamu, katika nchi mbali mbali mashariki ya kati.
Alioa mke wake wa kwanza akiwa na miaka 17, na baadaye akawaoa wake wengine wanne. Osama Bin Laden naaminiwa kuwa na watoto 17.

No comments: