Sunday, October 10, 2010

Afrika mwanao vipi na Ushoga?
Na Elia Migongo
JUNI 16 kila mwaka, bara letu la Afrika huadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika. Lengo la kuiadhimisha siku hii ni kuzikumbusha serikali za mataifa ya Afrika haja ya kumlinda mtoto wa Afrika kwa ajili ya ustawi wa bara letu.

Asili ya siku hii ni mauaji ya kinyama yaliyofanywa na iliyokuwa serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini Juni 16, 1976 huko Soweto, Afrika ya Kusini ambako wanafunzi kadhaa wa kiafrika waliuawa. Huko nyuma siku hii ilikuwa ikikumbukwa kwa kulaani kitendo kile cha kinyama cha Serikali ya Makaburu.

Kwa vile taifa la kesho la nchi yoyote ile litatokana na watoto wa leo, uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), sasa Umoja wa Afrika (AU) ulipitisha azimio kwamba siku hiyo ya Juni 16, itumike kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.

Yapo mambo kadhaa ambayo yakiachwa kuchipua katika jamii yatahatarisha ukuaji wa watoto hao hivyo kuharibu hali zao za baadaye. Hivi sasa lipo jambo baya na ovu kabisa ambalo linapigiwa chapuo la nguvu na Marekani na mataifa ya Ulaya Magharibi. Ovu hili ni ushoga.

Marekani na mataifa ya Ulaya Magharibi yamekuwa yakiisukuma Afrika katika maangamizi. Na sasa kasi hiyo imekuwa kubwa zaidi na ikichukua sura tofauti. Huko nyuma mataifa haya yalikuwa yakitumia ‘silaha’ ya kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe; na baada ya vita kulipuka, basi mataifa hayo huuza silaha kwa makundi yanayopigana ndani ya nchi husika. Hivi ndivyo ilivyokuwa nchini Msumbiji ambako RENAMO ilikuwa ikpambana dhidi ya serikali. Nchini Angola, serikali ilikuwa na wakati mgumu kupambana na kundi la Jonas Savimbi. Nchini Sudan, kundi la SPLA likiogozwa na John Garang limekuwa likiiyumbisha serikali ya nchi hiyo.

Marekani na Ulaya Magharibi tayari zimeitumbukiza Afrika katika ubaradhuli wa mashindano ya uzuri (beauty contest mfano Miss Tanzania) na Big Brother Africa! Afrika tayari tumenasa.

Sasa linapigwa chapuo la kuitumbukiza Afrika katika ushoga. Chapuo hili lilianza kidogo kidogo kwa majarida ya mtaani kuripoti vitendo vya kishoga Ulaya na Marekani. ‘Mdundo’ ulipozoeleka, chapuo likaongezwa nguvu kwa majarida hayo kuripoti matukio ya hapana na pale ya ushoga katika jami za kiafrika. Sasa chapuo linapewa nguvu zaidi kwa kuzituhumu nchi za Kiafrika zenye kupinga ushoga kwa madai kwamba “zinakiuka haki za msingi za binadamu”.

Tunawakumbusha viongozi wa serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengine wa nchi za Afrika kwamba ushoga ni uovu mkubwa na kitanzi cha hakika kwa ustawi wa mwanadamu. Ulaya na Marekani wana agenda yao ya kuitawala Afrika kwa wepesi.

Ushoga unakomesha kizazi. John na Alex wanapooana, tusitarajie mmoja wapo atashika ujazito, akajifungua na hivyo kufanya jamii ya mwanadamu iendelee kuwepo. Kadhalika, Maria anapomwoa Suzana, hapo haitapatikana mimba; na kama mimba hakuna, basi hakuna mwendelezo wa kizazi cha mwanadamu.

Athari za kubana kizazi zimeitia kiwewe Ulaya na Magharibi. Hivi sasa Ulaya inao wazee wengi kuliko vijana na watoto. Na tayari kasumba ya kutopenda watoto imewakolea wazungu kiasi kwamba serikali zao zinahaha kuirejesha hali ya wananchi kupenda kuzaa. Watu katika nchi hizo wanahimizwa kuzaana na wanaahidiwa zawadi mbalimbali, lakini kampeni hiyo hailekei kuzaa matunda.

Sasa balaa hilo wanalileta kwetu Afrika. Kwanza wanataka sisi tufanane nao katika msiba huo wa ukame wa watoto na vijana, na pili wanataka Afrika izorote ili vijana wao wachache watakaosalia Ulaya na Marekani wasipate taabu ya kuingia Afrika na kupora utajiri tulio nao.

Kufika hapa tunapenda kutoa pongezi za dhati na shukurani kwa utawala wa serikali Uganda kwa kuweka wazi kwamba ushoga ni jambo lisilokubalika nchini humo. Tunaziomba nchi zingine za Afrika ziitike mwangwi wa ndugu zetu Waganda.

Kwaupande mwingine tunailaani vikali hatua ya rais wa Malawi, Mutharika, ya kutambua ‘haki’ za mashoga kiasi cha kuwaachia huru wanaume wawili walipatikana na hatia ya kufunga ndoa ya jinsia moja.

Tunakamilisha maoni yetu haya kwa kukumbushia haja ya kumlinfda mtoto wa Afrika dhidi ya ubadharuli wa usenge n usagaji.

No comments: