Monday, October 4, 2010

Urais wetu na ndoa za mkeka
· Mwaka 1995 alikuwa Prof. Lipumba na mwaka 2010 ni Dkt. Slaa

Na Elia Migongo
UPO wimbo mmoja uliimbwa na bendi ya muziki wa Dansi inayomilikiwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania ya Mwenge Jazz,ambao ulitoka katikati ya miaka ya 1980 iitwayo Ndoa ya Mkeka.

WImbo huo unaeleza namna ndoa hizo ingawa hutambulika kama ndoa halali na jamii, zilivyo na mushkeri katika taratibu zake.

Unasema Ndoa ya mkeka haina mshenga, haina barua ya posa, wala haina sherehe za ngoma na burudani nyingine. Ni ndoa ambayo watu wengi huenda wasiwe na taarifa kwamba imefungwa, lakina inafungwa.

Kwa kawaida ndoa hii hufungwa kwa kushtukiza na ndugu wa mmoja wa maharusi wanaochoshwa na mchezo wa wahusika kuendelea na zinaa ilihali wangeweza kuhalalisha jambo hilo kwa kuwa wamechaguana wenyewe.

Huwashtukiza kwa kuwavamia wakiwa pamoja na kufanya taaratibu za harakaharaka kuhakikisha ndoa hiyo inafungwa mara moja.

Ndoa hizi hufungwa kwa taratibu za funika kombe mwanaharamu apite kwa nia ya kuwakinga wahusika na uendelezaji uzinzi.

Mara nyingi wanaokumbwa bna ndoa hizi ni vijana ambaio kutokana na kuzama kwenye maishaya ujana kiasi cha kuogopa kuitwa mume au mke, huendelea kufanya zinaa kwa kificho, ili mradi waendelee kutambulika kwamba hawajaolewa au kuoa.

Mbali ya wanaokwepa kuitwa mume au mke, wapo pia wanaogopa gharama za harusi na hata wanaoogopa gharama za mahari na nyinginezo muhimu kabla ya ufunga ndoa.

Ndugu na jama wa vijana husika huamua kuwafungisha ndoa ya mkeka vijana wao ili kuiepusha jamii yao na aibu ya vijana wao kufanya vitendo hivyo vya kukiuka mafundisho ya Mungu kwa kufanya zinaa.

Lakini si aghalab kukuta watu wazima wakijiingiza kwenye kundi la kufungishwa ndoa ya mkeka kwani kwa kawaida ndoa zao huwa ni za walioamua kufunga na si vinginevyo.

Hii ni kwa kuwa inaeleweka kwamba wazee huwa hawana cha kukwepa, si kuogopa kuitwa mume au mke, wala kukwepa gharama za harusi na sherehe. Na inapotokea mtu akakuta watu wazima wakifunga ndoa za mkeka, ndoa za siri, bila mialiko wala sherehe, ni lazima aingiwe na shaka na kilicho nyuma ya mipango ya kufunga ndoa za kijabu kama watoto wadogo.

Katika uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge wa mwaka 1995, kulikuwa na taarifa za kwamba mgombea urais kwa tiketi ya CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amepora mke wa mtu.

Taarifa hizo zilisema kwamba Profesa huyo hakuwa na ndoa na mwanamke huyo bali alimchukua tu mke wa mtu na kujifungisha ndoa ya harakaharaka ili kufunika kombe. Tofauti na funika kombe la vijana inayofanywa kwa lengo la kuwaondolea ndugu zao fedheha ya kushuhudia vijana wao wakifanya zinaa kinyume cha mafundisho ya dini, bali ni funika kombe mwanaharamu apite hasa.

Ni ndoa za harakaharaka kiasi kwamba siku zote huishia kwa wahusika kujikuta kwenye mizozo kwa kutokuwa makini kwao katika umiliki wa taratibu zao za maisha. Ni funika kombe yenye lengo la kuwaghilbu watanzania kwamba wao ni watu safi wenye familia zao wanazoishi nazo kwa amani na utulivu.

Lakini kwa kuwa waswahili husema harakaharaka haina baraka, ndoa hizo ziku zote huishia kwenye utata unaosababisha watu kuzilalamikia mahakamani na kudai fidia.

Ndoa kumbukumbu ya moja kwa moja, malalamiko dhidi ya ndoa ya Profesa Lipumba yaliishia wapi, lakini yalikuwepo ambapo mtu aliyedai kuwa na mke yule alitangaza kwenda mahakamani kumdai fidia Profesa Lipumba.

Mwaka huu, aibu hiyo imtjirudia na safari kwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Padre Wilbroad Slaa. Itakumbukwa kwamba Slaa ambaye ni kitaaluma na usomi wake ni Padre wa Kanisa Katoliki akiwa shahada ya udaktari, ya sheria za Kanisa (Cannon Law).
Ni ndani ya sheria hizi ambapo taratibu na umuhimu wa lazima kwa wakatoliki kufunga ndoa vimeelezwa. Lakini inaelezwa kwamba hata ndoia ya kwanza ya Padre Slaa, ilikuwa ya mkeka kwani haikupita kanisani kama ambavyo watu wangetarajia mtu wa usomi wa dini kama yeye na ambaye alikuwa na cheti cha kufungisha ndoa alichopewa na kanisa hilo kabla ya kutimuliwa na kanisa.
Lakini mara baaada ya kutangazwa kwamba ndiye mgomeba urais wa CHADEMA, padre naye akaamua kufunika kombe. Akautangazia umma wa watanzania kwamba anaye mwali mpya, aliyemuoa. Kama kawaida ya ndoa za mkeka, Padre Slaa hakusema ndoa hiyo alifunga wapi na lini.

Na kama ilivyo kawaida ya harakaharaka, Dlt, Slaa naye akakumbana na malalamiko ya kupora mke wa mtu, malalamiko ambayo hivi sasa kesi yake iko mahakamani na hivyo nisingependa kuzungumzia uhalali au uharamu wa ndoa hiyo ya Slaa.

Lakini kilichoshangaza ni kauli za kubabaika na hoja za nguvu za Dk. Slaa dhidi ya maalalamiko haya, akadai kwamba kwenye siasa za Tanzania hakuna mchafu na kwamba eti wakiendelea kumsema naye ataanika hadharani uchafu wao.

Ikazidi kushangaza kwa viongozi wa CHADEMA kudai eti madai yale ni njama za CCM, licha ya ukweli kwamba mlalamikaji alitoa hati ya ndoa ikiwa na jina la Mchungaji aliyeifungisha ndoa hiyo, pamoja na picha za ndoa. Lakini bado viongozi wa CHADEMA tena wengine wakiwa ni wanasheria wakadai eti malalamiko yale ni njama za CCM.

Hata hivyo unaporudi nyuma na kukumbuka kauli ya Slaa kwamba kwenye siasa za Tanzania hakuna mtu msafi na kwamba wakimwandama naye ataanika uchafu wao hadharani, inaonyesha namna hata yeye anavyokiri kwamba alimpata ndoa yule kwa njia za uchafu na ndio maana akatishia kuwaanika wenzake wa CCM ambao anajua ni wachafu kama yeye, ikiwa watanendelea kumwanika hadharani.

Hata hivyo, wenzake hao ambao hakuwataja majina, hawakushughulika na kauli yake kwani tangu mwanzo hawakuwahi kusema kwamba Padre Slaa amepora mke wa mtu, bali aliyesema na alinayedai kuporwa pamoja na watu wake wa karibu.

Hivi viongozi hawa wanaoamua kudanganya hata katika kufunga ndoa ambayo ni moja ya masuala muhimu katika binadamu, kwa kuamua kufunga ndoa kwa sababu tunaweza kuwaita nao ni makini. Mtu anayeshindwa kupanga mwenendo ya familia yake mapema, anaweza kweli kutuongoza na kutusaidia kupanga masuala ya nchi yetu.

Cha ajabu ni kwamba mapaka sasa, Si Padre Slaa waka wapambe wake waliosimama hadharani na kueleza kama Slaa anaoa wakati huu, hakuwahi kuwa na mke? Mke wake huyo wako wapi, anao wawili au amemwacha? Na kama amemwacha ni kwakuamua tu ama ni kwa nini.

Bado tunakumbuka kuhusu Padre huyu kufumainiwa na mkewe, ingefaa aeleze kwamba alimwacha mkewe aliyekuwa amkimtambulisha mwanzoni kutokana na kufumaniwa au kama aliamua tu na kuchukua chuma kingine.

Sitazungumzia kesi ya Mahimbo ambayo nasikia wiki ijayo itaanza mahakamani kwani najua fika kwamba hilo atalijibu hukohuko mahakamani.

No comments: