Wednesday, January 29, 2014

ULINZI UMEIMARISHWA HUKO TARIME, NI BAADA MAUAJI YALIYOTOKEA KWA SIKU MBILIMFULULIZO

Story ya Ahmad Nandonde, wa Jicho la mdadisi blog
SERIKALI imeimarisha ulinzi Wilayani Tarime Ambapo Jeshi la polisi Mkoa wa Mara na Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya kwa kushirikiana na kikosi cha Oparesheni Kutoka Makao Makuu ya Jeshi la polisi wanaendelea na zoezi la kuimarisha usalama na upelelezi dhidi ya jambazi lililouwa watu ambapo usiku wa kuamkia leo hakuna mauwaji yoyote yaliyotokea. Kutokana na hofu ya waanchi Usuku wa leo mida ya jioni wananchi walirejea majumbani kwao na watu kutoonekana wakitembea barabarani ambapo pia askari polisi wakiwa kwenye Difenda za polisi wamekuwa wakizungukazunguka kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Tarime wakiwa na mbwa kwa ajili ya kuimalisha usalama na msako mkali dhidi ya jambazi lisilofahamika ambalo limeuwa watu wapatao saba. Kamanda wa polisi Mkoa wa kipolisi Tarime Rorya Justus Kamugisha amesema jeshi la polisi limejizatiti vya kutosha kwa kuongeza askari kwa ajili ya msako nakwamba hawezi kusema kuwa kuna usalama wa kutosha nawakati jambazi bado halijakamatwa. Mkuuwa Wilaya ya Tarime John Henjewele amesema kuwa ulinzi wa kutosha umeimarishwa na tangu jumatatu msako uliongezeka baada ya kutokea mauwaji na msako umeongezwa kwenye Kata ya Turwa,Kitare,Binagi ambako matukio ya mauwaji yametokea na akawataka wananchi kutoa taarifa za siri pindi wanapopata dalili za mtu wasiye mjua anaingia kwenye maeneo yao.

STORY YA AWALI IKO HIVI...
HALI YA USALAMA TARIME IMEZIDI KUTOWEKA BAADA YA JAMBAZI LISILOFAHAMIKALIKIWA NA BUNDUKI AMBAYO HAIJAFAHAMIKA AINA YAKE KUENDELEA KUUWA WATU KWA RISASI KATIKA MAZINGIRA TOFAUTITOFAUTI AMBAO NI JINSIA YA KIUME NA IDADI YA WALIOUWAWA KUFIKIA SABA HADI SASA NA INADAIWA UUWA WATU NA KUPOTEA BILA KUTAMBULIWA. JAMBAZI HILO ISILOFAHAMIKA WATU NAUSIKU WA SAA MBILI JANUARI 27 /2014 MAENEO YA NKENDE LIMEMUUWA MWENDESHA BODABODA JUMA MARWA MKAZI WA NKENDE MJINI TARIME AKIWA ANAELEKEA NYUMBANI KWAKE AMABYE ALIKUFA AKIWA HOSPITALI AKIPATIWA MATIBABU. MGANGA WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI TARIME MARCO NEGA AMESEMA KUWA TANGU JANUARY 27 HADI SASA HOSPITALI IMEENDELEA KUPOKEA WATU WALIOUWAWA NA MAJERUHI AMBAO WAMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUGUNDULIKA WAKIWA WAMEJERUHIWA KWA RISASI KATIKA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI NAKWAMBA WATU WAPATAO 7 WAMEKUFA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA KIPOLISI TARIME/RORYA JUSTUS KAMUGISHA AMESEMA WAMEMKAMATA MTU MMOJA ANAESHUKIWA AMBAYE YUKO CHINI YA ULINZI KWA MAHOJIANO NAKWAMBA ANAZIDI KUONGEZA VIKOSI VYA DORIA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA TARIME. WANANCHI MJINI TARIME WALITAKA JESHI LA POLISI KUHAKIKISHA JAMBAZI LINAPATIKANA VINGINEVYO WALIOMBA JESHI LA POLISI LIWAKABIDHI WANANCHI BUNDUKI KUMSAKA JAMBAZI ANAYEFANYA MAUWAJI

No comments: