Bwana Ocharo,(Kulia) |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Mara imemsomea mashitaka ya kuharibu mali Diwani wa Kata ya Kigera Gabriel Ocharo(CUF) zenye thamani ya shilingi milioni 25,300,000 kinyume na kifungu cha 326 ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Imedaiwa na Mwendesha mashitaka Jonas Kaijage mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi Faisal Kahamba Diwani huyo kinyume na kifungu hicho alishiriki uharibifu wa majengo sita ya madarasa katika shule ya msingi Kigera A mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kutokana na kushindwa kukidhi masharti ya dhamana kulingana na thamani ya uharibifu uliofanyika katika shule hiyo,Ocharo alipelekwa rumande hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena februari 2 mwaka huu.
Hivi karibuni katika kikao cha Baraza la madiwani wa Halimashauri ya Mara
Hivi karibuni katika kikao cha Baraza la madiwani wa Halimashauri ya Manispaa ya Musoma lililofanyika chini ya Naibu Meya wa Halimashauri hiyo Bwire Nyamwero(Chadema) lililotoa agizo kwa Afisa Elimu Msingi wa Halimashauri hiyo kutoa taarifa polisi juu ya uharibifu wa majengo sita ya madarasa katika shule ya msingi Kigera A uliodaiwa kufanywa na Diwani huyo.
Kwenye kikao hicho, Diwani wa Kata ya Bweri Zidi Sondobhi(Chadema) alisema katika muhula huu wa masomo wanafunzi wa shule ya msingi Kigera A wameshindwa kuhudhulia vipindi madarasa kwa kile kilichoonekana majengo sita ya shule hiyo kung'olewa mabati na kushindwa kuezekwa hali inayofanya wanafunzi kushindwa kusoma na kuwaaomba madiwani watoe tamko la kumtaka Diwani huyo akamatwe.
Mkurugenzi wa Halimashauri ya Manispaa ya Musoma Ahmed Sawa alilieleza Baraza hilo hakuwa na barua yoyote wala kutoa maagizo ya kuondolewa mabati ya shule hiyo hali iliyomfanya Naibu Meya kuomba maelezo ya kina kutoka kwa Diwani wa Kata husika juu ya uhalibifu uliofanywa kwenye shule hiyo na baadae kutoa amri ya kufunguliwa mashitaka.
No comments:
Post a Comment