Leo katika chuo kikuu cha Mtakatifu
Agustino (SAUT)Kampasi kuu ya MWANZA , kumefanyika maonesho ya vitivo mbali
mbali vya chuo hicho katika siku maalumu inayojulikana kwa jina la SIKU YA SAUT
NA JAMII (SAUT COMMUNITY DAY).
Siku hii pamoja na mambo mengine huwa ni
utangulizi wa ya mahafali ya chuo hicho , kesho itakuwa ndio mahafali yenyewe .
Hii itakuwa mahafali ya 15 tangu chuo hicho kutunukiwa ama kubadilishwa kuwa
chuo kikuu kutoka iliyokuwa Taasisi ya mafunzo ya jamii Nyegezi (Nyegezi social
training Institute NSTI) mwaka 1998.
Vituvo mbali mbali vimeshiriki shughuli hii
ya leo vikiwemo Engineering, Mawasiliano ya Umma, Mahusiano ya Umma, Dini, Elimu,
Sayansi ya jamii na Philosohpia.
Mgeni rasmi katika shughuli hii ya leo
amekuwa na Askofu Ndimbo, Mwenyekiti wa Bodi ya chuo (SAUT), pamoja nae katika
meza kuu alikuwepo Makamu mkuu wa chuo hicho Dkt Pius Mgeni, Naibu makamu mkuu
wa chuo taaluma Dkt Thadeus Mukamwa na Dkt Helen , ambae ni mkuu wa masomo ya
shahada za juu.
Hivihapa baadhi ya picha za tukio zima siku
ya leo..
Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma Dkt Mukamwa |
Wataalamu wa picha mnato wakiwa kazini |
Dkt Pius Mgeni |
Sr Helen |
WATAALAMU WA MAJENGO NA UMEME
BURUDANI KATIKA MASHAIRI NA UTUNZI TUNDUIZI...picha ya chini wataalamu hawa waliamua kucheza wimbo wa MAJANGA wa Snura
WATAALAMU WA REDIO
Chini: Bi Martha na Bwana Innocent wakiwa tayari kuelekeza uhariri wa picha za video
KUKABIDHI SHAIRI KWA MGENI RASMI
Bi Ester Lymo, hapa akishughulika na kamera |
Maelekezo kabla ya kuingia banda la PCCB na AISEC
WATAALAMU WA USHAURI NASAHA KUTOKA HOSPITALI YA BUGANDO
WATAALAMU WA UTETEZI WA UHAI - PRO LIFE
WATAALAUMU WA MAZINGIRA
WATAALAMU WA MAWASILIANO YA UMMA UPANDE WA REDIO
Bwana Haji Yona (mwenye sahati la draft) akitoa ufafanuzi juu ya utangazaji |
Fr Mwanga Tiago, Joseph Kigingi (wa kwanza na wa pili kulia) wakitoa ufafanuzi juu ya uhariri wa vipindi vya redio |
Mtaalamu kutoka kitengo cha mainjinia wa umeme akifafanua jambo |
Bwana |Elia Migongo akimfafanulia mgeni rasmi juu ya urushaji wa matangazo katika redio |
Bwana Said Lufune (aliyevaa Headphone) akitoa ufafanuzi juu ya uchanganyaji wa picha katika luninga |
Bwana Godfriend Mbuya(aliyekaa) hapa akimuelekeza mgeni rasmi na jopo lake juu ya usomaji wa habari wa luninga |
No comments:
Post a Comment