Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 3091
wamehitimu katika vitivo mbali mbali , huku wengi zaidi ya 800 wakishindwa
kuhitimu kutokana na sababau mbali mbali zikiwemo kushindwa kufisha alama
stahiki za ufaulu katika mihula yao mbali mbali.
Shughuli hiyo ilianza kwa ibaada ya misa
takatifu, ambapo wahitimu na wanajumuiya wengine walihudhuira misa hiyo ambayo
iliongozwa na Baba Askofu Niwemugizi wa jimbo la Lulenge Bukoba.
Aliyetunuku vyeti stashahada , shada na
shahada za uzamili alikuwa ni makamu wa rais wa baraza la maaskofu katoliki (TEC)
Askofu Niwemugizi wa jimbo katoliki la Bukoba. Wageni wengine mahususi walikuwa
ni pamoja na jaji mkuu mstaafu jaji Agustino Ramadhani, na majaji wengine wa
kanda ya mwanza, viongozi wa serikali.
Yafuatayo ni baadhi ya matukio katika picha..
Picha ya kwanza na ya pili katika misa takatifu. Picha ya tatu ni Jaji Agustino Ramadhani akishiriki katika Misa hiyo |
Hitimisho la misa takatifu. Picha ya chini ni brass band ikiongozi wahitimu na wahadhri pamoja na jukwaa kuu kuingia uwanjani katika mahafali |
Ndugu zangu katika taaluma wakijitahidi kuweka mambo sawa |
President wa wanafunzi Bwana Dova akitoa neno kidogo |
Maaskofu Niwemugizi (Kulia) na Askofu Ndimbo wakiendelea kutafakari na kufuatilia mambo katika mahafali hiyo |
Makam mkuu wa chuo SAUT Dkt Pius Mgeni akitoa neno katika kusanyiko hilo |
Kijana wangu kutoka radio SAUT FM Martini Nyoni ... akinukuu machache wakati alipoongoza matangazo ya moja kwa moja |
Hoyce Temu katika mahojiano na radio SAUT FM mapema leo |
Mhariri mkuu wa kwa Neema Fm, ya Mwanza Bwa Jeston Kihwelo akiwa na wake wa ubani mara baada ya kuhitimu shahada ya mawasiliano ya umma |
2 comments:
Kazi nzuri
Karbu sana kaka Dova
Post a Comment