IBARA 94.-(2) Watu wafuatao hawatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa mawaziri au naibu mawaziri katika serikali ya jamhuri ya muungano:
(a) Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Wabunge wa Bunge la Tanzania Bara, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar au madiwani kutoka Washirika waMuungano;
(b) mtu aliyewahi kutiwa hatiani kwa makosa ya ubadhirifu wa mali za umma, ama katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanzania Bara au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
SIFA ZA MTU KUWA WAZIRI NI ZIPI KWA MUJIBU WA IBARA HII....ni hizi
94.-(1) Mtu atateuliwa kuwa Waziri
au Naibu Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano ikiwa:
(a) ni raia wa
kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria za nchi;na
(b) angalau ana
shahada ya kwanza ya Chuo Kikuu kinachotambulika kwa mujibu wa Sheria za
nchi.
....>>> SHIDA HAPA NI HAWA MAWAZIRI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WATAPATIKANAJE ?>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KUTOKA KWA MAONI YA DOTTO BULENDU... UCHAMBUZI WAKE UKO HIVI..
Ibara ya 75(e) ya
rasimu inasema ili kugombea nafasi ya uraisi ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,mgombea anatakiwa kuwa
na sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hii;
Kwa mujibu wa Ibara ya 117(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea kuchaguliwa kuwaMbunge-(a) ikiwa mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatuvya miaka mitano!.......
Kwa mujibu wa Ibara ya 117(2) Mtu hatakuwa na sifa za kugombea kuchaguliwa kuwaMbunge-(a) ikiwa mtu huyo aliwahi kuwa Mbunge kwa vipindi vitatuvya miaka mitano!.......
KWA MUJIBU WA MAONI YA DOTTO,...kama Ibara hii itaanza kuhesabu kuanzia sasa,Dk
Silaa,Lowasa,Sitta na Membe hawatakuwa na sifa za kugombea Uraisi........je hii
Ibara tumeiona?wale mlioko kwenye mabaraza hebu waulizeni watu wa tume
wanamaanisha nini?
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>IBARA YA 92
(3) Baraza la Mawaziri ndicho chombo kikuu cha kumshauri Rais
kuhusu mambo yanayohusu utekelezaji wa madaraka na matumizi ya
mamlaka ya Rais.
(4) Bunge
naMahakama hazitakuwa na uwezo wa kisheria
kuchunguza kama ushauri wowote
au ushauri wa aina gani ulitolewa na Baraza la Mawaziri.
No comments:
Post a Comment