Wednesday, August 28, 2013

UELEWA MDOGO UNAKWAMISHA UCHANGIAJI WA MAONI KWA WALEMAVU

Story ya Ahmad Nandonde , MUSOMA
Imeelezwa Kuwa Uelewa Mdogo Na Muda Mdogo Wa Kujadili Katiba Ni Miongoni Mwa Changamoto Zinazowakabili Watu Wenye Ulemavu Mkoani Mara.

Hayo Yamesemwa Jana Na Katibu Mkuu Wa Chama Cha Kusaidia Watu Wenye Matatizo Ya Akili Tuspo Bw. Shukrani Bwire Wakati Wa Kikao Cha Baraza Cha Kujadili Rasmu Ya Katiba Mpya.

Bwire Amesema Kutokana Na Katiba Kuandikwa Kitaalamu Hivyo Watawatumia Wataalamu Wawezeshaji Ili Kuhakikisha Wanaichanganua Katiba Ili Iwafikie Walengwa Ipasavyo.

Aidha Amesema Kutokana Na Watu Hao Kukabiliwa Na Matatizo Hilo Ni Wazi Kuwa Wamewatumia Wazazi Au Walezi Katika Kuchangia Suala Zima Uchangiaji Maoni Ya Katiba Mpya.


Kwa Upande Wake Katibu Mwenezi Wa Tuspo Bw. Shukrani Egubo Ameitaka Jamii Na Watu Wanaohusika Kuwsaidia Watu Wenye Magonjwa Ya Akili Kuendelea Kutoa Maoni Ili Kuwawezesha Kupata Haki Ya Msingi Na Hivyo Kuondoakana Na Tabia Ya Kutlekezwa Na Jamii Zao.

No comments: