Maelfu ya wana-Arumeru Mashariki waliohudhuria wakati CHADEMA wakizindua
kampeni zao, kwa ajili ya uchaguzi mdogo
HAYA NI BAADHI YA MAMBO AMBAYO ZITO KABWE ALIYASEMA SIKU HIYO... 10 March
"Uchaguzi wa Ubunge Arumeru Mashariki ni kipimo cha namna wananchi navyoridhika na watawala, namna mnavyoridhika na mgawo wa Ardhi na namna mnavyoridhika na mgawanyo wa Maji katika Wilaya yenu".
ANACHOAMINI MBUNGE HUYO WA KIGOMA KASKAZINI....
"Wawekezaji wanapewa Ardhi na mtaji!Haya ndio yanajenga hasira ya wananchi wa Meru. Hasira hii kwa vyovyote itahamishiwa katika sanduku la kura ili kumpata Mbunge kutoka miongoni mwao atakayeweza kusimama kidete kuhakikisha Ardhi inapatikana kwa wananchi wa Meru.
Kwa nini huko nyuma, katika chaguzi zilizopita Jambo hili halikuwapa hasira wananchi? Ni dhahiri hapakuwa na Mwanasiasa ambaye ana uwezo mkubwa wa kulieleza na kuwapa imani wananchi. Ndugu Joshua Nassari amedhihirisha kwamba analijua tatizo hili kwa dhati kabisa.
Nilivyomsikiliza akiongea katika kampeni, na pia katika mazungumzo yetu binafsi amenithibitishia kuwa ni mwanasiasa kijana mwenye kipaji kikubwa katika kujenga hoja na ku articulate masuala ya msingi.Changamoto nyingine kubwa kwa Meru ni haki ya kupata Maji.
Meru kuna Maji mengi sana lakini matajiri wenye mashamba wameyazuia Maji hayo na hivyo wananchi wa kawaida hawapati Maji ya kumwagilia mazao Yao na pia kwa matumizi ya nyumbani.
Hili nalo linajenga hasira kubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Ardhi na Maji ni masuala yanayokwenda pamoja wilayani Meru.Mwisho kabisa nimeona makundi ya vijana wasio na ajira na hivyo kukosa Kipato. Vijana wengi wanashinda kwenye stendi za mabasi na kuita abiria.
Ukosefu wa Ajira kwa vijana Kama tusemavyo kila wakati ni changamoto kubwa sana kwetu viongozi na hasa viongozi vijana..................'' MWISHO WA NUKUU....
INGAWA hatima ya nini na nani wakuiongoza Arumeru Mashariki, ni kwa wananchi wenyewe wa Arumeru hiyo ya Mashariki.... nadhani ni wakati ambao watanzania wanahitaji kuutumia kwa makini sana... na kuweza kufanya chaguo ambalo halitawajutisha wao.
AMANI ITAWALE...
|
No comments:
Post a Comment