Thursday, December 5, 2013

RORYA WAASWA KUJIJENGEA TABIA KULINDA NA KUTUNZA MAZINGIRA.

Na Ahmad Nandonde , MUSOMA.


RORYA.
WANANCHI WILAYANI RORYA WAMEASWA KUJIJENGEA TABIA YA KULINDA NA KUTUNZA MAZINGIRA ILI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.
 Mratibu mradi wa elimu ya mazingira katika bonde la ziwa victoria W.W.F BW. Kelvin Robert akizungumza na waandishi wa habari
HAYO YAMESEMWA JANA NA MRATIBU MRADI WA ELIMU YA MAZINGIRA KATIKA BONDE LA ZIWA VICTORIA LINALOTEKELEZWA NA W.W.F BW. KELVIN ROBERT KATIKA KILELE CHA MADHIMISHO YA SIKU YA UTOAJI WA ELIMU YA JUU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA ILIYOFANYIKA WILAYANI RORYA KATIKA VIWANJA VYA OBWERE SHIRATI.

AMESEMA KUWA WILAYA YA RORYA NA BUTIAMA NI MIONGONI MWA WILAYA ZILIZOATHIRIKA KWA KIASI KIKUBWA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA HII INATOKANA NA UKATAJI MITI WA MARA KWA MARA NA HIVYO KUPELEKEA MVUA KUTIRIRIKA NA KUSABABAISHA MAFURIKO.

MBALI NA KUWAHIMIZA WANANCHI KUPANDA MITI KWAAJILI YA KUTUNZA MAZINGIRA LAKINI PIA UPANDAJI MITI IKIWA NI PAMOJA NA KUYATUMIA MAGUGU MAJI KAMA SEHEMU YA KUINUA KIPATO CHAO HATA KATIKA SHUGHULI MBALI MBALI.


NAYE DIWANI WA KATA YA MKOMA KWA TIKETI YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA BW. AGTOR LAZARO AMEKIRI KUYTOKE KWA HALI HIYO YA MABADILIKO YA TABIA NCHI NA HIVYO HALMASHAURI KUAMUA KUWEKA SHERIA NDOGO NDOGO ILI KUKOMESHA TABIA YA UKATAJI WA MITI HOVYO ILI KUDHIBITI WAKATAJI MITI NA HATA WAUZAJI WA MIKAA ILI HATUIA IWEZE KUCHUKULIWA.
KWA UPANDE WAKE MKAZI WA ENEO HILO BI. BENADINA NYAMBITA AMESEMA TATIZO HILO LA MABADILIKO YA TABIA NCH YAMETOKANA NA TABIA YA BAADHI YA WATU KUKATA KATA MITI HOVYO KWAAJILI YA MKAA NA ULIMAJI WA PEMBEZONI MWA ZIWA VICTORIA NA HIVYO KUATHIRI KWA KIASI KIKUBWA SHUGHULI ZA KILIMO.

HATA HIVYO HIVYO AMEWAOMBA WANANCHI KUJITOLEA KATIKA UPANDAJI MITI ILI KUSAIDIA UPATIKANAJI WA MVUA NA HIVYO KUONDOKANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI.                                           

                         

No comments: