Thursday, December 5, 2013

ALIEJIFANYA USALAMA WA TAIFA JELA MIAKA MITATU


Na Ahmad Nandonde, MUSOMA.
MAHAKAMA YA WILAYA YA MUSOMA IMEMUHUKU KWENDA JELA MIAKA MITATU MTU MMOJA AMBAYE AMEFAHAMIKA KWA JINA LA LISSU CHACHA MARWA MKAZI WA WILAYA YA TARIME KWA KUPATIKANA NA KOSA LA KUJITAMBULISHA AU KUJIITA AFISA USALAMA TAIFA KUTOKA MAKAO MAKUU JIJINI DAR ES SALAAM.

KATIKA HUKUMU HIYO ILIYOTOLEWA JANA NA HAKIMU MKAZI NA MFAWIDHI YA MAHAKAMA HIYO MHE. RICHARD MAGANGA AMESEMA AWALI MTUHUMIWA HUYO ALIJITAMBULISHA KUWA NI AFISA USALAMA WA TAIFA BAADA YA KUFIKA KWENYE OFISI ZA MWANDISHI WA HABARI WA REDIO ONE NA ITV ZILIZOPO KATIKA MTAA WA DILUX BW. GEORGE MARATO NA KISHA KUJITAMBULISHA KWA CHEO HICHO.

AIDHA AMESEMA BAADA YA MTUHUMIWA HUYO KUFIKA KWENYE OFISI HIZO ALIHOJIWA NA MWANDISHI HUYO AMBAYE ALIMTILIA SHAKA BAADA YA KUONEKANA KUTOZIFAHAMU OFISI ZA USALAMA WA TAIFA MKOA.

HAKIMU MAGANGA AMESEMA MTUHUMIWA HUYO AMEDAI KUWA SABABU YA YEYE KUFIKA MKOANI HAPA NI KWAAJILI YA KUFUATILIA MTANDAO WA WAUZAJI SILAHA NA RISASI KUTOKA KWENYE KIKOSI CHA KG MAKOKO KILICHOPO MANISPAA YA MUSOMA HALI ILIYOPELEKEA KUANZA MARA MOJA KAZI ILIYOMLETA KITU AMBACHO KILIBAINIKA KUWA NI UONGO NA HII NI KUTOKANA NA UTENDAJI WAKE WA KAZI KUTOFAUTINA NA MAJUKUMU YALIYOMLETA.

AKITOA HUKUMU HIYO HAKIMU MKAZI WA MAHAKAMA YA WILAYA YA MUSOMA MHESHIMIWA RICHARD MAGANGA MBELE YA MWENDESHA MASHITAKKA WA SERIKALI PP STEPHANO MGAYA AMESEMA KUWA MAHAKAMA IMEFIKIA UAMUZI HUO WA KUMHUKUMU MTUHUMIWA MIAKA MITATU MARA BAADA YA KUJILIDHISHA NA USHAHIDI ULIOTOLEWA NA MASHAHIDI SABA MAHAKAMANI HAPO.

KUFUATIA HIKUMU HIYO BAADHI YA WANANCHI WAMEKUWA NA MTAZAMO TOFAUTI TOFAUTI JAMBO AMBALO WAMESEMA KUWA NI CHANGAMOTO KWA VYOMBO VYETU VYA USALAMA.

No comments: