Thursday, November 14, 2013

STORY MBILI KUTOKA MUSOMA LEO...HIZI HAPA

Story za Ahmad Nandonde
MUSOMA. MKUU WA WILAYA YA MUSOMA BW. JACKSON MSOME AMEWATAKA MAAFISA WATENDAJI WOTE WILAYANI HAPA KUSHIRIKI KIKAMILIFU NA KWA WAKATI KATIKA ZIARA YA MKUU WA MKOA INAYOTARAJI KUFANYIKA HIVI KARIBUNI KATIKA WILAYA YA MUSOMA. AKIZUNGUMZA NA MAAFISA HAO KATIKA UKUMBI WA HALIMASHAURI YA MANISPAA, MSOME AMEWATAKA WALE WOTE WANAOHUSIKA NA KAMATI YA MAANDALIZI YA ZIARA HIYO KUWAJIBIKA KIKAMILIFU IKWEMO NA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA MAENEO AMBAYO MKUU HUYO WA MKOA ATAYAPITIA KATIKA ZIARA HIYO ITAKAYODUMU KWA TAKRIBANI SIKU TATU MFULULIZO. MSOME AMESE SISITIZA KUWA NA KUWATAKA MAAFISA AFYA KWA KUSHIRIKIANA NA WATAALAMU WA AFYA, MADIWANI PAMOJA NA VIONGOZI WA KATA NA MITAA KULITAZAMA UPYA SUALA LA USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA KATIKA ZIARA YA MKUU WA MKOA KATIKA HALI YA AMANI. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
BUTIAMA. MJANE WA BABA WA TAIFA MAMA MARIA NYERERE, AMESEMA ENDAPO KILA KIONGOZI ATATEKELEZA KWA VITENDO KAULI MBIU YA KILIMO KWANZA KWA KUANZISHA MASHAMBA YA MFANO KATIKA VIJIJI WANAVYOTOKA KUNAWEZA TASAIDIA KWA KIASI KIKUBWA KULETA MABADILIKO YA HARAKA KATIKA SEKTA HIYO. MAMA MARIA NYERERE AMEYASEMA HAYO KATIKA KIJIJI CHA BUSEGWE WILAYANI BUTIAMA BAADA YA KUTEMBELEA SHAMBA DARASA LENYE MAZAO YA MAHINDI NA MIGOMBA AMBALO LIMELIMWA NA MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJI MH NIMROD MKONO KAMA MFANO KWA WANANCHI WENGINE KATIKA ENEO HILO. AMESEMA KUWA KUTOKANA NA MABADIRIKO YA TABIANCHI KILIMO CHA UMWAGILIAJI KWA KUTUMIA MABONDE KINA NAFASI KUBWA YA KUPUNGUZA TATIZO LA NJAA NA UMASIKINI NCHINI LAKINI YOTE HAYO YATAWEZEKANA TU ENDAPO VIONGOZI WATAACHA SIASA NA KUONYESHA MFANO KATIKA KUFANYA MABADILIKO HAYO KATIKA SEKTA YA KILIMO. HATA HIVYO MJANE HUYO WA BABA WA TAIFA AMESEMA ILI SEKTA YA KILIMO IWEZE KUCHOCHEA KASI YA UKUAJI WA UCHUMI NI LAZIMA WANANCHI WAKAKUBALI KULIMA KWA KUFUATA USHAURI WA WATALAAM WA UGANI KUTAWAWEZESHA KULIMA ENEO DOGO NA KUPATA MAVUNO MAKUBWA NA HIVYO KULIWEZESHA TAIFA KUJITOSHELEZA KWA CHAKULA NA KUPUNGUZA TATIZO KUBWA LA NJAA. SHAMBA HILO LA MAHINDI NA MIGOMBA AMBALO LIMEONEKANA KUMVUTIA MAMA MARIA NYERERE LIMEKUWA LIKITUMIKA NA WANANCHI WA KIJIJI HICHO KAMA DARASA KWA KUJIFUNZA KILIMO BORA KWA KUTUMIA PEMBEJEO ZA KISASA IKIWA NI PAMOJA NA MATUMIZI YA MBOLEA

No comments: