Thursday, October 31, 2013

UGALI WA MUHOGO WAGHARIMU MAISHA YA WATOTO WAWILI MKOANI MARA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA. WATOTO WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA CHACHA BONIFAS (6) NA BONIFAS JOSEPH (3) WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KULA UGALI WA MUHOGO UNAODHANIWA KUWA NA SUMU BAADA YA KUNUNUA UNGA HUO KATIKA GHALA LA MKAZI MMOJA KIJIJINI HAPO. AKITHIBITISHA KUTOKEA KWA VIFO HIVYO KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI MARA ACP FERDINAND MTUI AMESEMA MNAMO TAREHE 28 MWEZI OCT. MAJIRA YA SAA 6:00 WATOTO HAO AMBAO NI WATOTO WA BW. JOSEPH MKAZI WA KIJIJI CHA BUSWAHILI WILAYANI BUTIAMA WALIKUMBWA NA UMAUTI BAADA YA KULA CHAKULA HICHO KINACHODHANIWA KUWA NA SUMU . KAMANDA MTUI AMESEMA SAMBAMBA NA TUKIO HILO , MTOTO MWINGINE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MWITA JOSEPH (8) AMEKIMBIZWA KATIKA HOSPITALI YA MUSOMA BAADA YA KULA CHAKULA KILICHOPIKWA NA UNGA HUO. KUFUATIA TUKIO HILO JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA BI. MAGDALENA JOSEPHATI MMILIKI NA MFANYABIASHARA WA GHALA LILILOKUA LIKITUMIKA KUHIFADHIA UNGA HUO. AIDHA KAMANDA MTUI AMETOA WITO KWA WANANCHI KUWA WAANGALIFU PINDI WANAPOHIFADHI VYAKULA VYAO HUSUSAN KWENYE MAGHALA IKIWA NI PAMOJA NA KUTOCHANGANYA MADAWA YA AINA YEYOTE ILI KUEPUSHA MADHARA YATAKAYOJITOKEZA.

No comments: