Saturday, May 11, 2013

KAMA HUKUISOMA STORI YA MTOTO ALIEUAWA NA POLISI KWENYE HARAKATI...HII HAPA

Mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi rebu wilayani tarime mkoani mara deus jacob,ameuawa kinyama baada ya kupigwa risasi kichwani na askari polisi wa wilayani tarime wakati wakiwa katika harakati za kumkamata mtuhumiwa wa kosa la kushambulia na kujeruhi.

kamanda wa polisi kanda maalum ya tarime rorya,kamishina msaidizi justus kamugisha,amesema mwanafunzi huyo mkazi wa songambele wilayani tarime amepigwa risasi hiyo ambayo imesababisha kupoteza maisha na askari polisi mwenye namba d 4662 koplo methew wakati akipita barabarani.

kamanda kamugisha amesema kuwa risasi hiyo ambayo imemuawa mwanafunzi huyo ni miongoni mwa risasi tano ambazo zilifyatuka wakati wa porukushani ikihusisha mtuhumiwa huyo marwa chacha na askari polisi katika jaribio la kupora bunduki.

kwa mujibu wa kamanda kamugisha askari polisi huyo anashikiriwa kwa mahojiano wakati wakimtafuta mtuhumiwa marw chacha ambaye alikimbia baada ya tukio hilo kutokea ambapo polisi walifanikiwsa kukamata misokoto ya bangi 45 na kilo 3 na roba za bangi kavu ambayo inadaiwa ni mali ya mtuhumiwa huyo.

kwa upande wake mzazi wa mwanafunzi huyo mzee jacob mwita sasi,amelaani kitendo cha polisi huyo kumua mtoto wake kwa risasi bila kosa hivyo kutaka vyombo vya sheria kuchukua harua ili kuhakikisha haki inatendeka.
,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,,,//,,,,,,,,,,//,,,,,

SUMATRA-MUSOMA

UMOJA wa wafanyabiashara wa Usafirishaji mkoani Mara,wamelalamikia kitendo cha Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na Majini SUMATRA mkoa wa Mara kwa ukiukwaji wa sheria namba 8 ya mwaka 2007 ya Mamlaka hiyo kwa kuruhusu na kupangia safari magari ambayo hayana leseni ya kusafirisha abiria.

Katika barua yao iliyoandikwa kwenda kwa Meneja wa SUMATRA mkoa wa Mara ambayo Radio One Stereo imepata nakala yake imedai inashangazwa na Mamlaka hiyo kukiuka sheria ambazo inazisimamia kwa kuruhusu mambo ambayo yanakwenda kinyume cha utaratibu kwa kuruhusu magari hayo na hivyo kuwanyonya wenye leseni halali.

Barua hiyo imesema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilalamikia suala hilo kwa kufikisha taarifa maeneo husika lakini hakuna hatua zozote ambazo zimekwisha kuchukuliwa na Mamlaka yoyote kutokana na ukiukwaji wa sheria.

Sehemu ya barua hiyo imesema hata walipoona Sumatra inashindwa kulichukulia hatua suala hilo wamekwenda katika vyombo vingine ikiwemo kikosi cha usalama barabarani lakini hadi leo hakuna hatua iliyochukuliwa.

Katika barua hiyo ambayo nakala yake ilipelekwa kwa kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mara pamoja na ofisi ya Mamlaka ya Mapato TRA ililikalili gari namba T 930 BVW aina ya Toyota Costa linalofanya safari kati ya Majita na Musoma linalodaiwa kuwa la mfanyabiashara maarufu mkoani Mara limekuwa likifanya biashara ya usafirishaji wa abiria kwa muda mrefu bila kufuata taratibu za kisheria.

Dereva hao walidai huenda kuna kitu cha chini ambacho kinafanyika baina ya wamiliki wa magari hayo pamoja na maofisa wa Sumatra na mamlaka nyingine kwa kuwa suala hilo licha ya kulilalamikia lakini bado wamelikalia kimya na kushindwa kuchukua hatua zozote.

Akizungumza na Radio One Stereo kuhusiana na malalamiko hayo,Meneja wa Sumatra mkoa wa Mara Bw Michael Rogers,amekili kuwepo kwa gari lililotajwa namba zake likifanya kazi bila kufuata utaratibu na tayari ameshawasiliana na vyombo vingine vya usalama kufatilia malalamiko hayo.

Hata hivyo amekiri kuwa gari namba T 930 BVW Toyota Costa imelikuta likiwa limebeba abiria maeneo ya Musoma Mjini tayari kuelekea Majita Busekera Wilaya ya Musoma Vijijini huku likiwa halina stika za Sumatra wala bima na nikaliamulu kushusha abiria mbele ya polisi na kupelekwa kituoni kwa hatua zaidi.

No comments: