Saturday, March 16, 2013

WANAWAKE JITOKEZENI KUPIMA SARATANI

Story ya Ahmad Nandonde MUSOMA.

WANAWAKE MKOANI MARA WAMEOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI ILI KUEPUKA MAGONJWA YA KIZAZI KWA WANAWAKE.
AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA HOSPITALI YA MKOA SISTER MARGARET ISHENGOMA AMEELEZA KUWA NI MUHIMU KWA WANAWAKE KUJITOKEZA KUPIMWA NA KUPATA CHANJO YA VIRUS VYA PAPILOMA(HPV) ILI KUZUIA SARATAN YA SHINGO YA KIZAZI.

AMESEMA KUWA VIASHIRIA HIVYO VYA HPV NI HATARI ZAIDI KWANI VINAWEZA KUKAA MWILINI KWA ZAIDI MIAKA 10 BILA KUONESHA DALILI ZAKE.
WANAWAKE WALIO NA UMRI CHINI YA MIAKA 52 NDIO WAATHIRIKA WAKUBWA WA SARATAN YA SHINGO YA KIZAZI.
NA MWISHO AMETOA USHAURI KWA WANAWAKE WA MKOA WA MARA KUZINGATIA NAFASI HII YA UPENDELEO KWANI HUDUMA HII HAINA MALIPO NA WOTE WAFIKE KATIKA HOSPITALI YA MKOA KWA MATIBABU NA USHAURI ZAIDI.

No comments: