Friday, February 1, 2013

MSICHANA WA MIAKA 20 ABAKWA NA KUAWA, MUSOMA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA
Msichana Mmoja Mwenye Umri Wa Miaka 20 Jina Linahifadhiwa Mkazi Wa Buhare Amebakwa Na Kisha Kuuawa Na Watu Wasiojulikana.
Akidhibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo, Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mara Kamishina Msaidizi Mwandamizi Bwana Absalom Mwakyoma Amesema Msichana Huyo Baada Ya Kufanyiwa Unyama Huo , Mwili Wake Umepatikana Maeneo Ya Buhare Jana Tarehe 31 January , 2013 Saa Kumi Na Robo Jioni Na Kupelekwa Katika Hospitali Ya Mkoa Wa Mara.
Amesema Watu Hao Walimfunga Nywele Zake Katika Mti Na Kisha Kuchana Chana Nguo Zake Za Ndani Na Kisha Kutekeleza Ukatili Huo Wa Kinyama Na Wa Kusikitisha.
Aidha Kamanda Mwakyoma Ametoa Wito Kwa Wananchi Kuamka Na Kuwafichua Wale Wote Wanaohusika Na Mauaji Hayo Kwani Wapo Katika Jamii Zinazowazunguka Ili Wakamatwe Na Kufikishwa Mbele Ya Sheria.
Katika Tukio Lingine Leo Asubuhi Huko Mwigobero Karibu Na Feri Majira Ya Saa Saba Na Dakika Kumi Asubuhi Mwanaume Mmoja Mwenye Umri Unaokadiriwa Kuwa Kati Ya Miaka 65 Hadi Miaka 70 Umepatikana Ukielea Ziwani.
Akidhibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Kamanda Wa Polisi Kamishina Mwandamizi Msaidizi Bwana Absalom Mwakyoma Amesema Mwili Wa Mwanaume Huyo Umekutwa Akielea Juu Ya Maji Akiwa Amekufa Tayari Na Inasadikika Alikuwa Amekwenda Kuoga.
Amesema Mwili Huo Baada Ya Kuopolewa Ulikutwa Hauna Alama Yoyote Ya Majeraha Na Mfukoni Alikuwa Na Dodoki La Kuogea , Chanuo, Sabuni Ya Kipande , Na Noti Ya Shilingi 500.
Aidha Kamanda Mwakyoma Amesema Mwili Huo Umefifadhiwa Katika Hospitali Ya Mkoa Wa Mara .

No comments: