Tuesday, February 26, 2013

JAMAA ACHOMWA KISU SEHEMU ZA SIRI, AFARIKI DUNIA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA.
MTU MMOJA ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JOSEPH WALESI MKAZI WA SHINYANGA VIJIJINI AMEUWAWA KWA KUCHOMWA NA KISU SEHEMU ZAKE ZA SIRI NA WATU WASIOJULIKANA.

AKITHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO KAMANDA WA POLISI MKOA WA MARA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI ABSALOM MWAKYOMA AESEMA KUWA TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 24 MWEZI WA PILI MWAKA HUU MAJIRA YA SAA 2:00 USIKU KATIKA KIJIJI CHA MAGUNGA, KATA YA MIRWA TARAFA YA MAKONGORO WILAYANI BUTIAMA.
AIDHA JESHI LA POLISI LIMEWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA SIRI KWA VYOMBO VYA SERIKALI KWA WALE WALIOHUSIKA NA MAUAJI HAYO YA KINYAMA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
AMESEMA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILO BADO HAKIJAJULIKANA HADI SASA NA KWAMBA POLISI WANAEDELEA NA UCHUNGUZI ILI KUFAHAMU CHANZO CHA MAUAJI HAYO.

No comments: