Tuesday, February 26, 2013

CLOUDS YAPIGWA FAINI MIL 5, KWA NEEMA FM NA IMAAN FM ZAFUNGIWA


 

KUTOKA MTANDAO WA CLOUDS FM WAMEANDIKA HIVI...


Serikali kupitia kamati ya Maadili ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imevifungia kwa muda wa Miezi Sita vituo vya Redio vya IMAAN ya Mkoani Morogoro na Radio KWA NEEMA ya mkoani Mwanza, kutokana na kukiuka kanuni na taratibu za utangazaji kinyume na Sheria namba 5 ya Utangazaji ya Mwaka 1993.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo WALTER BIGONYA amesema kwa nyakati tofauti vituo hivyo vimekuwa vikishiriki kurusha matangazo ambayo yamekuwa yakileta uchochezi kwa jamii, ambapo kituo cha Redio IMAN kimedaiwa kushiriki kuhamasisha watu wasishiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi huku kituo cha redio cha KWA NEEMA kikishiriki kueneza uchochezi juu ya suala la kuchinja baina ya wakristo na waislamu.
Kufuatia hali hiyo BIGONYA amevitaka vyombo vya Habari nchini kuepuka matumizi mabaya ya vyombo hivyo kwa kueneza chuki na uchochezi katika jamii, na kuongeza kuwa Vyombo vya habari vikitumika vibaya vina nafasi kubwa ya kuleta machafuko katika nchi.
Katika Hatua nyingine Kamati hiyo imekipiga Faini ya Shilingi Milioni Tano Kituo cha Redio cha CLOUDS FM, kufuatia kurusha matangazo yanayoashiria uhamasishaji wa vitendo vya ushoga, kupitia kipindi chake cha Asubuhi cha POWER BREAKFAST kilichokwenda hewani Januari 23 Mwaka huu.


KUTOKA JAMII FORUM

Radio hizi mbili zimefungiwa miezi sita, na Clouds FM kupigwa faini ya milioni 7
KWA NEEMA FM Mwanza: Sababu ni kushabikia maswala ya uchinjaji Mwanza
Radio Iman FM Morogoro: Kushabikia watu kutoshiriki Sensa 2012Clouds FM:
-Kuendesha/kushabikia masuala ya ushoga wakati wa uchaguzi wa Marekani, kuendesha kipindi cha uchochezi wakati wa uchaguzi wa Marekani.
-Kuendesha kipengere cha 'Jicho la ng'ombe' kisichofuata maadili.
TCRA kitego cha mahudhui ndio kimefanya kazi hii leo.
CHANZO: Jamii Forum

No comments: