Monday, January 14, 2013

WIKI TATU ZA MWAKA 2013 , FUNZO LA MWALIMU MWAKASEGE HILI HAPA


Tunaanza leo wiki ya 3 ya mwaka huu wa 2013, kwa kusema na wewe juu ya nguvu iliyomo katika Jina la Yesu. Jina la Yesu Kristo lina nguvu sana. Lakini ili nguvu hizi zionekane kwako unapolitumia inabidi imani yako juu ya jina la Yesu iongezeke.
Wakati fulani katika kitabu cha Matendo ya Mitume sura ya 3, watu waliwauliza akina Petro jinsi walivyoweza kumsaidia mtu aliyekuwa kiwete tangu azaliwe hata akaweza kutembea. Jambo hili liliwashangaza sana waliomfahamu kiwete huyo, maana wakati anaupata muujiza huo wa kutembea alikuwa na miaka zaidi ya 40. Petro akawajibu akasema" Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu,amemtukuza mtumishi wake Yesu.... na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemuona na kumjua na imani ile iliyo kwake yeye imampatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote" ( Matendo ya Mitume 3:13,16)
Ni dhahiri Mtume Petro alitaka wale waliokuwa wanamsikia wakati ule ya kuwa jina la Yesu lina nguvu za Yesu ndani yake! Na imani waliyokuwa nayo juu ya jina hilo ilifanya nguvu zile zijidhihirishe na kufanya kile walichotamka kwa jina la Yesu kitamkwe.
Kiwango cha imani yako juu ya Jina la Yesu kikoje? Je unapolitumia jina la Yesu,unaona matokeo ya kile ulichotamka au ulichoomba kikitokea?
Tunakutakia wiki njema huku ukilitafakaro jina la Yesu na uwezi uliomo ndani ya ndani ya jina hili.
Like ·  ·  · 6 hours ago · 

No comments: