Thursday, January 24, 2013

DC MUSOMA AWAPONGEZA MADIWANI

Story ya Ahmad Nandonde , MUSOMA
MKUU WA WAWILA YA MUSOMA JACKSON MSOME AMEWAMWAGIA SIFA MADIWANI WA HALIMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA AMBAO WENGI WAO WANATOKANA NA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KWA KUWA MSTARI WA MBELE KUSIMAMIA MASLAHI YA UMMA IKIWEMO MAHINDI YA CHAKULA CHA BEI NAFUU YALIYOTOLEWA NA SERIKALI.

MSOME AMETOA KAULI HIYO ALIPOKUWA AKIHITIMISHA WIKI YA ELIMU YA WATU WAZIMA KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII BUHARE NA KUSEMA KITENDO CHA UWAJIBIKAJI KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO ZINAPASWA KUUGWA MKONO.
AMESEMA KATIKA KUFUTILIA CHAKULA CHA BEI NAFUU KILICHO TOLEWA NA SERIKALI KATIKA KUKABILIANA NA NJAA MADIWANI HAO WAMEKUWA MSITARI WA MBELE KATIKA KUHAKIKISHA MANISPAA YA MUSOMA AMBAYO IMEDAIWA KUWA NA NJAA KUBWA INAPATA CHAKULA CHA KUTOSHA.
MSOME AMESEMA MADIWANI WOTE WAMEKUWA KITU KIMOJA KATIKA KUFUATILIA SUALA HILO NA KUHAKIKISHA MANISPAA YA MUSOMA INAPATA TANI MIANNE KATI YA MIATISA ZA MAHINDI ZILIZO TOLEWA NA SERIKALI KUTOKA GHALA LA TAIFA LA KUHIFADHI MKOANI SHINYANGA KUJA MKOANI MARA KATIKA KUKABILIANA NA UHABA WA CHAKULA.
AMESEMA TAYARI MAHINDI YA CHAKULA AMBAYO YANAINGIZWA KATIKA MANISPAA YA MUSOMA KUTOKA KWA WAFANYABIASHARA WALIO TEULIWA NA KUUZWA KWA BEI AMBAYO INAELEKEZWA NA SERIKALI AMBAPO KILO MOJA YA MAHINDI INAZWA KLWA BEI YA SHILINGI MIASABA HUKU KILO MOJA YA UNGA WA SEMBE IKIUZWA KWA SHILINGI MIATISA.
MKUU HUYO WA WILAYA AMEWATAKA MADIWANI WA MANISPAA YA MUSOMA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUFUATILIA UUZWAJI WA MAHINDI HAYO ILI WANACHI WASIUZIWE KWA BEI ZAIDI KUTOKA KWA WAFANYA BIASHARA AMBAO WAMETEULIWA.
AIDHA MKUU HUYO WA WILAYA AMEWATAKA WANACHI KUTOA USHIRIKIANO KWA VIONGOZI PALE WATAKAPOONA WAFANYABIASHARA WANAUZA MAHINDI HAYO KWA BEI YA JUU ILI WACHUKULIWE HATUA KALI ZA KISHERIA.

No comments: