WIKI MOJA BAADA YA KUTEMBELEA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA MKOA ILIYOPO MUSOMA MJINI WAFANYAKAZI WA RADIO VICTORIA FM KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBALI MBALI MKOANI HAPA MCHANA WA LEO WANATEMBELEA KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA VILIVYOPO WILAYANI HAPA IKIWA NI PAMOJA NA KUTOA MISAADA MBALI MBALI.
AKIZUNGUMZA NA RADIO VICTORIA FM MCHANA HUU MRATIBU WA SHUGULI HIYO BW. PATRICK DERICK MWANKALE AMESEMA KUWA HATUA HIYO INALENGO LA KUWAWEKA KARIBU WATOTO HAO NA KUWAFANYA WAJISIKIE KAMA WATOTO WENGINE WAISHIO MAJUMBANI NA WAZAZI WAO.
AIDHA BW. MWANKALE AMESEMA MATEMBEZI HAYO YATAENDANA SANJARI NA UGAWAJI WA ZAWADI MBALI MBALI KWA WATOTO HAO IKIWEMO MCHELE, SABUNI ZA KUFULIA, MADAFATARI, PENSELI, KATONI ZA MAJI YA KUNYWA , MABOKSI YA BISKUTI IKIWA KAMA MOJA YA SEHEMU YA KUSHEREHEKEA SIKU YA KRISSMAS NA MWAKA MPYA.
AWALI KWA UPANDE WAKE MRATIBU WA KIPINDI CHA ELIMIKA NA WATOTO (UMABU) KINACHORUSHWA KILA SIKU YA JUMAAPILI NA RADIO VICTORIA FM BW. BURUDE NDAGO AMESEMA KITENDO KILICHOONESHWA NA MWANKALE CHA KUANDAA MATEMBEZI HAYO NI KITENDO CHA KIBINAADAMU ZAIDI KWANI WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU HAWAKUPENDA KUWA KATIKA HALI HIYO BALI NI MIPANGO YA MWENYEZI MUNGU.
HATA HIVYO BW. BURUDE AMEWATAKA WATU WENGINE KUWA NA MOYO KAMA HUO KWANI KWA KUFANYA HIVYO KUTAWEZESHA KUFANIKISHA MASLAHI YA MTOTO NA USTAWI WA MTOTO AMBAO NI MSINGI WA MAISHA YENYE MAFANIKIO.
MIONGONI MWA VITUO VINAVYOTEMBELEWA MCHANA HUU NI PAMOJA NA KITUO CHA JIPE MOYO KILICHOPO MAENEO YA MWISENGE NA ST. JUSTINE KILICHOPO MAENEO YA MAKOKO.
No comments:
Post a Comment