Tuesday, December 25, 2012

UJUMBE MZITO WA XMASS KUTOKA KWA MWALIMU CHRISTOPHER MWAKASEGE


Mimi na mke wangu na familia yetu yote- yaani watoto ma wajukuu, tunakutakia siku njema ya krismasi.
Ujumbe nilionao kwako ni Mathayo 2:1-23. Ndani ya ujumbe huu napenda kukuambia mambo mawili makubwa
Jambo la Kwanza,
Yesu Kristo alipozaliwa Bethelehemu, si kila mtu alifurahi. Biblia inasema ya kuwa kuzaliwa kwa Yesu kuliposikika: " Mfalme Herode....alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye"(Mathayo 2:3). Kwa hiyo, hata wewe usishangae unapoona si kila mtu anafurahi juu ya kuokoka kwako. Si kila mtu atafurahi atakapoona Yesu anazaa kitu moyoni mwako. Na pia usitegemee kuona kila mtu anayekuona unadumu katika Kristo atakufurahia
Jambo la Pili,
Kama vile Mungu alivyomsaidia na kumlinda Yesu alipozaliwa asiuwawe na wale waliochukia kuzaliwa kwake,uwe na uhakika Mungu huyu atakilinda kilicho cha Yesu katika maisha yako, kisiuwawe na wanaokichukia.
Naamini ujumbe huu utakutia moyo katika siku hii muhimu.
Like ·  ·  · 2 hours ago · 

No comments: