Sunday, December 30, 2012

MAKAMPUNI YATAKIWA KUSAMBAZA MBEGU ZA PAMBA MAPEMA

Story ya Ahmad Nandonde, BUNDA

SERIKALI IMEYATAKA MAKAMPUNI YANAYOSAMBAZA MBEGU YA ZAO LA PAMBA ZA MAJARIBIO MKOANI MARA KUHARAKISHA KUTOA MBEGU HIZO KWA MKOPO KWA WAKULIMA KABLA YA MSIMU WA KUPANDA ZAO HILO HAUJAISHA.
 
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS,MAHUSIANO NA URATIBU MH STEPHEN WASSIRA,AMETOA AGIZO HILO WILAYANI BUNDA MKOANI MARA,AMBAPO AMETAJA MAKAMPUNI HAYO YANAYOSAMBAZA MBEGU HIYO KUWA NI OLAM TANZANIA LTD, ALLIANCE LTD NA S&C LTD.
 
AMESEMA KUWA MBEGU HIYO NI TOFAUTI NA MBEGU ZA PAMBA ZA HAPO AWALI HIVYO SERIKALI IMETEUA MKOA WA MARA KUZALISHA MBEGU HIYO KWA MAJARIBIO ILI BAADAYE IWEZE KUSAMBAZWA KWA WAKULIMA WA MIKOA MINGINE NA KUTOFANYA HIVYO NI KUVURUGA ZOEZI HILO MUHIMU KWA KILIMO CHA ZAO LA PAMBA.
 
AKIWA ZIARANI BUNDA WAZIRI HUYO AMEPOKEA MALALAMIKO KUTOKA KWA WAKULIMA JUU YA KUWAPO KWA BAADHI YA MAKAMPUNI YANAYOSITA KUWAPATIA WAKULIMA MBEGU HIYO KWA MIKOPO HUKU WAKIJUA WAZI KUWA WALISHAKUBALIANA NA SERIKALI KUFANYA HIVYO.
BAADHI YA WAKULIMA KATIKA VIJIJI MBALIMBALI HADI JANA WAMELALAMIKA KUWA HAWAJAPATA MBEGU HIYO YA KISASA INAYOUZWA KWA SHILINGI 1200 KWA KILO WAKATI AMBAPO MSIMU WA UPANDAJI UNAMALIZIKA.
 
KWA UPANDE WAKE KAIMU AFISA KILIMO WILAYA YA BUNDA BW BENSON BUTULI,AMEWATAKA WAKULIMA WA WILAYA HIYO KUTOPANDA MBEGU TOFAUTI NA HIYO INAYOSAMBAZWA AINA YA UK.91 KWA SABABU ITASABABISHA MIKANGANYIKO WAKATI WA UKUSANYAJI WA MBEGU HIYO.
 
KWA SABABU HIYO AMEWATAKA MAOFISA UGANI WA KILIMO VIJIJINI KUTOA MAELEKEZO SAHIHI KWA WAKULIMA KUHUSU MCHAKATO WA UPATIKANAJI NA UPANDAJI WA MBEGU HIYO YA UK.91 KUANZIA HIVI SASA.

No comments: