Mwandishi na mtaalamu wa masuala ya kimataifa, SAMMY AWAMI |
Kinachotokea hivi sasa Misri, kinapigia mstari swali langu la muda mrefu juu ya kuwapa nafasi wapinzani kuongoza nchi.
Lakini labda kabla sijaendelea sana, niseme tu kwamba mimi si mfuasi wa chama chochote kile. Kuna baadhi ya mambo ya CCM yanatia kichefuchefu sana, lakini pia kuna mienendo fulani ya chadema inatia shaka sana kama kweli niamue kuwapigia kura waingie Ikulu. Ni maoni yangu tu.
Siku chache zilizopita, Rais wa Misri Mohamed Morsi alieteuliwa hivi karibuni tu alitangaza kujipatia mamlaka makubwa kupindukia, kwamba hata Mahakama, chombo cha msingikabisa cha kusimamia haki na usawa, kisingeweza kumuhoji katika maamuzi yake.
Lakini ni miezi kadhaa tu iliyopita, Morsi alikua upande wa upinzani akiungwa mkono na wananchi wengi hata wakamuondoa Mubarak madarakani. Yeye na wananchi, ambao amewasaliti kwa tangazo lake, walipigania sana jambo hilo hilo, kwamba Mubarak alijitwika madaraka makubwa. Kaingia ikulu, amesahau kabisaaaa!!
Swali langu: Ni kweli kwamba CCM mmetukatisha tamaa wananchi kwa kiasi kikubwa sana tu. LAKINI JE..., WHY SHOULD I TRUST CHADEMA FOR MY COUNTRY!!???
No comments:
Post a Comment