Wednesday, November 14, 2012

CCM, NI JK TENA, MANGULA KUMSAIDIA BARA, SHEIN ZANZIBAR
SHEIN 100%, MANGULA 100% na JK 99.92%STORY KIDOGO HII HAPA
Matokeo ya nafasi za makamu mwenyekiti Zanzibar na Tanzania Bara yatangwazwa rasmi,ambapo hakuna kura iliyoharibika hivyo wamepita kwa asilimia 100%.
Dr. Ali Mohamed Shein ,Rais wa Zanzibar amepita kwa idadi ya kura 2397 na hakukuwa na kura za hapana, hivyo kutangazwa rasmi kuwa ndio Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,wakati huo huo Philip Mangula amechaguliwa kwa kura 2397, hakuna zilizoharibika ,hivyo Mh. Mangula ndio Makamu Mwenyekiti mpya kwa upande wa Tanzania Bara.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Mwenyekiti  wa CCM kwa kura  2395 kati ya 2937 zilizopigwa  ambazo ni sawa na asilimia 99.92%
PICHA : CCM blog

No comments: