Sunday, October 28, 2012

SYRIA MAKUBALIANO YAMEWASHINDA

Mapigano yamepamba moto nchini Syria licha ya makubaliano ya kuweka chini silaha katika siku kuu ya Idd Al Adha.Upande wa upinzani unazungumzia kuhusu  mapigano yaliyoenea kote nchini kati ya waasi na vikosi vya serikali.Watu wasiopungua 20 wameuwawa.
Kwa mujibu wa wanaharakati wa Syria,makubaliano hayo ya siku nne yaliyoanza kufanya kazi tangu Ijumaa iliyopita,yameshavunjwa mara 220.
Mapigano yameripotiwa pia kati ya jamii ya Waarabu na ile ya Wakurdi..Vikosi vya serikali ya Syria vilimuahidi mpatanishi wa kimataifa Lakhdar Brahim,vitaheshimu makubaliano hayo kwa sharti, kwamba vitajibu shambulio lolote la waasi.
Masharti kama hayo yalitolewa pia na waasi.Habari za hivi punde zinasema madege ya kivita ya serikali yanahujumu vitongoji vya mji mkuu Damascus.

STORY YA DW

No comments: