Sunday, October 28, 2012

MBABE WA HAMAS AUAWA

Mpiganaji wa chama cha Hamas ameuliwa kufuatia hujuma za madage ya kivita ya Israel.Mwanaharakati mwengine amejeruhiwa.Wote hao wawili walikuwa wakiendesha pikipiki karibu na Khan Yunes madege ya kivita ya Israel yalipowavurumishia mabomu.Hujuma hizo zimejiri siku tatu baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa na pande hizo mbili,kabla ya siku kuu ya Iddi l Adha.
Kabla ya hapo maguruneti 80 yalivurumishwa  toka Gaza dhidi ya Israel.Israel ilijibu kwa hujuma za angani na kuwauwa Wapalastina wanne.

STORY YA DW

No comments: