Saturday, October 27, 2012

SIMBA YAILAZA AZAM 3 -1 UWANJA WA TAIFA LEO

Emmanuel Okwi ,mabao yake mawili yameizamisha Azam katika uwanja wa Taifa , baada ya timu ya SIMBA kuibuka na ushindi wa 3-1. Awali John Bocco aliendeleza ubabe wake dhidi ya kipa mahiri nchini Juma Kaseja baada ya bao lake la mapema dakika ya 5 na kuifanya Azam iongoze, kabla ya Felix Sunzu kusawazisha katika ya 7. Okwi alipigilia msumali wa pili kabla ya half time kabla ya kufunga bao la tatu katika dakika 51. 
Kwa matokeo haya ya leo , Simba sasa inajikita kileleni mwa ligi, huku Azam ikishuka hadi nafasi ya tatu baada ya ushindi wa leo wa Yanga dhidi ya JKT Oljoro. Bao la Yanga limefungwa na Mbuyi Twite katika dakika ya 53.

No comments: