Story na Ahmad Nandonde
Halmashuri Ya Mkoa Wa
Mara Imetakiwa Kuepuka Kutegemea Harambee Kutoka Mikoa Ya Mbali Kama Vile Dar
Es Salaam Badala Yake Watumie Wananchi Waishio Mkoa Huo Na Wadau Mbalimbali Wa
Maendeleo Ili Kuchangia Harambee Ya Muendelezo Wa
Ujenzi Wa Hospital Ya Kwangwa Ambayo Itaitwa Mwalimu Nyerere Memorial Hospital.
Hayo Yamesemwa Mjini
Musoma Katika Kikao Cha Ushauri Cha Mkoa Rcc Kilichofanyika Katika
Ukumbi Wa Mkoa Huo Ambapo Kiasi Cha Shilingi
Bilioni Tano Zinahitajika Ili Kuakamilisha Ujenzi Huo Na Tayari Serikali
Imetenga Shilingi Bilioni Mbili Kwa Ajiri Ya Ujenzi Huo Hivyo Kuwepo
Na Upungufu Wa Shilingi Bilioni Tatu Ambazo Ndizo Zitakazofanyiwa Harambee.
Ujenzi Na
Harambee Hiyo Unatarajiwa Kuanza Rasmi Hivi Karibuni Na
Hii Imekuja Siku Chache Baada Ya Taarifa Ya Mkakati Wa Mkoa Wa Mara Wa
Kuboresha Huduma Za Afya Za Rufaa Katika Ngazi Ya Mkoa Iliyotolewa Na Mganga
Mkuu Wa Mkoa, Na Kujadiliwa Na Kikao Cha Kamati Ya Ushauri Ya Mkoa Rcc Ambapo
Wajumbe Mbali Mbali Walipendekeza Hoja Zitakazo Hakikisha Kuwa
Ujenzi Huo Unaanza Rasmi Ikiwa Ni Pamoja Na Ukusanyaji Wa Fedha Za Kuendeshea
Hospitali.
Sanjari Na Hayo
Wajumbe Pia Waliomba Kuundwa Kwa Bodi Ya Hospital Ya Mkoa Ambayo Itatoa Msaada
Mkubwa Katika Kuendeleza Huduma Za Tiba,Vilevile Uchangiaji Wa Uendeshaji Wa
Hospital Ya Kwangwa Unatarajia Kufanyika Jijini Dar Es
Salaam Na Mjini Musoma ,Ambapo Mkuu Wa Mkoa Wa Mara Mhe John Tuppa
Amemtaja Mhe Rais Kuwa Mgeni Rasmi Katika Harambee Iyo.
Kadhaika Wajumbe
Wameomba Tathmini Ya Fidia Kwa Watakaoathirika Na Uendelezaji Wa Hospitali Iyo
Ya Kwangwa Ifanyike Na Ukamilke Mapema Na Pia Tathmini Ionyeshe Kuwa Ni Kaya
Ngapi Zitalipwa Fidia Na Kiasi Gani Cha Pesa Kitakacholipwa Kwa Kila Kaya.
No comments:
Post a Comment