Friday, September 7, 2012

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWAHAMASISHA AKINA-BABA KUSHIRIKI SUALA LA AFYA YA UZAZI

Story imeandikwa na Ahmad Nandonde, alieko PWANI 

Waandishi Wa Habari Nchini Wametakiwa Kuandika Habari Zitakazoibua Mijadala ambayo Itawafanya Wanaume Kushirikishwa Katika Suala Zima La Afya Ya Uzazi Wa Mpango.

Hayo Yamesemwa Leo na Dk.Katanta Simwanza Alipokuwa Akizungumza Na Waaandishi Wa Habari Katika Semina Ya Siku Tatu Inayofanyika Mjini Bagamoyo.

Dk.Simwanza Amesema Endapo Mwanaume Atashirikisha Ataweza Kutoa Mchango Mkubwa Katika Jamii Husasani Sula La Uzazi Wa Mpango Kutokana Na Uwezo Wa Kutoa Maamuzi Alionano Katika Jamii Na Hata Hali Ya Kujiamini.

Aidha Dk.Katanta Amewataka Watu Kutokuwa Na Dhana Inayoamini Kuwa Wanaume Ni Waonevu Na Ni Watu Wabaya Kwa Jamii Na Kuwataka Kuaachana Na Dhana Hiyo Kwani Wanaume Ni Wakishirikishwa Wanaweza Kuleta Mabadiliko Katika Suala La Afya Uzazi Wa Mpango.

Akizungumzia Suala La Sera Ya Afya Bi.Beatrice Ezekiel Ameitaka Serikali Kujipanga Ili Kufanikisha Utekelezaji Wa Sera Ya Jinsia Ili Kuweza Kuleta Mabadiliko Katika Jami Na Hii Ni Kutokana Na Baadhi Ya Halmashauri Klatika Dawati La Jinsia Limekuwa Likikikumbwa Na Changamoto Zitokanazo Na Ukosefu Wa Vitendea Kazi Na Fedha.

Ameongeza Kuwa Ili Kutekeleza Sera Ni Lazima Srekilali Kkutenga Kiasi Cha Fedha Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwa Utaratibu Wa Kuwawezesha Wanahabari Kupata Taarifa Sahihi Na Kwa Kawati Ili Waweze Kufikisha Taarifa Kwa Jamii Husika.

Hata Hivyo Kwa Upande Wake Mwezeshaji Mwengine Katika Semina Hiyo Bw. Sospeter Magumba Amesema Tatizo La Jinsi Limekuwa Likiwaelemea Zaidi Wanaume Kutokana Na Kujihusisha Na Mambo Mengi Ya Kuisaidaia Famili Hali Inayomfanyakushindwa Kushiriki Ipasavyo Katika Suala Zima La Upangaji Wa Uzazi Wa Mpango.

Semina Hiyo Imeeandaliwa Na Shirika La Kimataifa La Nchini Ujerumani La Giz Kwa Lengo La Kuelimisha Waandishi Wa Habari Masuala Mbali Mbali Ya Jinsi Jinsia Na Maambukizi Ya Virusi Vya Ukimwi.

No comments: