Saturday, September 22, 2012

UNAMJUA ALIETIMULIWA LEO YANGA

NI KOCHA WAO MBELIGIJI...... wanasema ametofautiana na sera zao....STORY KIDOGO HII HAPA
KOCHA Mbelgiji Tom
Saintfiet amefukuzwa kazi usiku huu, baada ya kutofautiana sera na uongozi wa
Yanga na sasa Fredy Felix Minziro, aliyekuwa Msaidizi wake, atakaimu nafasi
yake.
Jana mchana, uongozi
wa Yanga ya Dar es Salaam, ulitangaza kuisimamisha kazi Sekretarieti nzima ya
klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu,
kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.


Makamu Mwenyekiti wa
Yanga, Clement Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya
Utendaji kilichofanyika tangu saa 5:30 hadi saa 9:30 hiyo jana.

No comments: