Monday, August 27, 2012

MWENYEKITI WA CCM MTWARA ASEMA HATATETEA NAFASI YAKE KATIKA UCHAGUZI WAO

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mtwara, Alhaji Dadi Mbulu ametangaza rasmi kutotetea nafasi yake katika uchaguzi wa chama hicho unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo (Agosti, 27,2012) ofisini kwake Mbulu alisema hana mpango wa kutetea kiti chake kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.

Mbulu ambaye alisema katika kipindi cha uongozi wake hatasahau alivyosakamwa na baadhi ya wanachama wake kwa kutoa ‘kifungoni’ mbunge wa Mtwara Mjini Hasnain Murji baada ya kufungiwa na viongozi waliopita wa chama hicho alisema.

“Nimechuja …Nimepata maamuzi kutoendelea kutetea kiti changu…kubwa zaidi afya yangu, pia kama kiongozi lazima niwe na moyo wa kuridhika, nimekuwa mwenyekiti wa halmashauri na meya kwa miaka 11 na mwenyekiti wa CCM  kwa miaka Mitano, sasa inatosha”

Aliongezakuwa “Hakuna shinikizo kutoka kwa mtu yeyote…katika kipindi

changu nimeweza kuimarisha chama na nashukuru naondoka madarakani  chama kikiwa tawala…hapa mkoani uchaguzi wa vitongoji mwaka 2009 tulishinda vitongoji 2672 kati ya 3122, vijiji  576 kati ya 1076 na mwaka 2010 tulishinda kata 136 kati ya 149 na wabunge wote saba ni wa CCM”

Alishauri kuwa ni vema kwa wagombea kujiepusha na kampeni za kuchafuana kwani zinaweza kusababisha mgawanyiko wa chama hata baada ya uchaguzi.

“Kuna dalili za kuchafuana….huko kufilisika kisiasa, wasitumie nafasi hiyo kuchafua majina ya wengine…jieleze utakifanyia nini chama na si kushambulia wagombea wenzako” alisema Mbulu
Habari kwaniaba ya Kusini blog

No comments: