Sunday, July 15, 2012

KWA MUHUTASARI YAHUSUYO TAARIFA YA UTENDAJI WA VIONGOZI WA BUNGE


Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa shughuli za Bunge na mijadala ya Wabunge juu ya mahitaji ya umma kwao kwenye maendeleo, uongozi, kuimarisha utawala bora, uwajibikaji wa serikali na haki za binadamu na kuimarisha usimamizi wao kwa serikali kupitia mijadala yao katika vikao vya Bunge. Taarifa hii inahusika na utendaji wa viongozi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2011.
Kwa Ujumla:
Kumekuwa na upendeleo wa vyama katika kujadili na kuchangia hoja na kuonekana Mh Spika na Wenyeviti wa vikao kutumia vibaya kanuni za bunge kuwadhibiti wabunge kulingana na vyama vyao. Mfano ni pale Mh Spika alipomzuia Mh Tundu Lissu kumwuliza swali Mh Mizengo Pinda juu ya mauaji ya raia mikononi mwa vyombo vya dola kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani juu ya hoja hiyo. Pamoja na Mh Lissu kujitahidi kufafanua tofauti zilizopo kati ya kesi inayomkabili yeye na wenzake na hoja anayoiulizia, bado Mh Spika ameendelea kuizuia hoja hiyo. Kulingana na maoni ya wabunge 36, Watendaji 22, wachambuzi 11 na wananchi 48 waliohojiwa, ubora wa uongozi wa bunge  kwa mwaka 2011 ni kama ilivyo hapa chini:

No comments: