Monday, July 16, 2012

18 WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUMUUA MWENYEKITI WA UVCCM SINGIDA


Jeshi la polisi mkoa wa Singida linawashikilia wakazi 18 wa kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi kwa tuhuma ya kumuua mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) Yohana Mpinga (30) baada ya kumpiga kwa kutumia silaha za jadi.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Vicent Sinzumwa amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 14 katika kijiji cha Ndago.
Amesema siku ya tukio, Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kilikuwa na kibali halali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha Ndago na mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa mbunge wa jimbo la Ubongo jijini Dar-es-salaam.
Sinzumwa amesema mara baada ya CHADEMA kuanza mkutano huo, viongozi wake walianza kuporomosha mvua ya kashifa mbalimbali dhidi ya mbune wa jimbo hilo Mwingullu Nchemba, kitendo ambacho kiliudhi baadhi ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.
Kamanda huyo amesema kuwa vurugu hizo zilihusisha kundi la wanachama wa CHADEMA na wa CCM na zilisambaa ambapo wanachama hao walianza kurusha mawe ovyo na askari wachache wa polisi waliokuwepo, walizidiwa nguvu na makundi hayo.
Amesema katika kundi hilo ambalo wamelikamata,watawahoji na wataobainika kuhusika watafikishwa mahakamani wakati wowote.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
KUSHIKILIWA KWA AFISA SERA WA CHADEMA

Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia Afisa wa sera na utafiti wa Chama cha CHADEMA Makao Makuu Waitara Mwita Mwikwabe, kwa tuhuma ya mauaji ya mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi Yohana Mpinga (30).
Kiongozi huyo wa CHADEMA alikamatwa muda mfupi baada ya kumaliza kutoa tamko la chama hicho kutokuhusika na mauajio ya kijana huyo kiongozi wa CCM kwa waandishi wa habari.
Waitara, mbunge wa jimbo la ubungo jijini Dar -es- salaam Mh. John Mnyika na mshauri wa CHADEMA na Mhadhiri wa chuo kiku cha Dar- es- salaam Dk. Kitila Mkumbo, inadaiwa walichochea mauaji hayo kwa kitendo chao cha kumkashifu mbunge wa  wa jimbo la Iramba magharibi Mwigulu Lameck Nchemba.
Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Linus Vicent Sinzumwa, kashifa hizo zimetolewa na viongozi hao wa CHADEMA, Julai kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi, pia karibu kabisa na kituo kidogo cha polisi cha Ndago, ambapo viongozi hao wanatuhumiwa kutoa kashifa hizo dhidi ya Mwigullu.
Sinzumwa amesema baada ya viongozi hao kuacha kueleza sera za chama chao na kuanza kumkashifu Mwigullu, baadhi ya wananchi waliwataka kuacha mara moja kumkashifu mbunge wao, lakini  viongozi hao walipuunza maombi hayo ya wananchi.
CHANZO, MO blog

No comments: