Friday, June 22, 2012

WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI HUU HAPA


Jumuiya Yetu sote tuilinde, 
Tuwajibike tuimarike,
Umoja wetu ni nguzo yetu,
Idumu Jumuiya yetu. 

1. Ee Mungu twakuomba ulinde,
Jumuiya Afrika Mashariki,
Tuwezeshe kuishi kwa amani,
Tutimize na malengo yetu. 

2. Uzalendo pia mshikamano,
Viwe msingi wa Umoja wetu,
Natulinde Uhuru na Amani,
Mila zetu na desturi zetu. 

3. Viwandani na hata mashambani,
Tufanye kazi sote kwa makini,
Tujitoe kwa hali na mali,
Tuijenge Jumuiya bora.

No comments: