Sunday, June 24, 2012

WASEMAVYO WAPINZANI (KAMBI RASMI) KUHUSU BAJETI MBADALA

Waiziri Kivuli, mambo ya fedha na uchumi
Upinzani wowote makini lazima uwe na uwezo wa kutoa mawazo tofauti, hatuwezi kuwa watu wa kulalamika tu bila kuonyesha sisi tungefanya nini. Tumekuwa tunatoa Bajeti Mbadala kila mwaka tangu mwaka 2007 na mafanikio yamekuwa makubwa sana. Tumeboresha hotuba zetu mwaka hadi mwaka na hoja zetu zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kuboresha Mapato. Changamoto kubwa sana tuliyonayo ni namna bora ya kusimamia uwajibikaji katika matumizi ya Serikali ambayo yanakua siku hadi siku.


Mwaka jana katika Bajeti mbadala, tulishauri kuhusu tozo ya SDL itumike kugharamia elimu ya Juu. Serikali ilichukua wazo hili. Mwaka huu tumependekeza kwamba tozo hii pia itolewe na Mashirika ya Umma, Serikali imekubali. Mabadiliko haya yataingiza zaidi ya Tshs 320bn na kuweza kulipia mikopo wanafunzi takribani 120,000 ikiwemo fedha kwa ajili ya VETA.
Mwaka jana katika Bajeti mbadala tulipendekeza kutunga sheria kuzuia makampuni makubwa ya nje yanayouziana 'assets' zilizopo Tanzania bila kulipa kodi. Mwaka huu Serikali imetekeleza wazo hili. Kuanzia sasa mauzo ya rasilimali zetu yaliyokuwa yanafanywa holela sasa yamezuiwa kisheria. Changamoto ni utekekezaji kutokana na ufisadi uliokithiri katika mfumo wa Serikali na wakusanya mapato.
Kuna jumla ya mapendekezo 10 katika Bajeti Mbadala ya mwaka huu yamekubaliwa na Serikali. Tunatendelea kutoa mawazo zaidi ili kuboresha nchi yetu na kuwaonyesha Watanzania kuwa tukikabidhiwa dola tunaweza kuendesha nchi bila mashaka yeyote.

No comments: