Wednesday, June 6, 2012

VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA

Tel: +255 22 21122065/7                                                                      Ofisi ya Bunge
FaxNo. +255 22 2112538                                                                     S.L.P. 941
Email:tanzparl@parliament.go.tz                                                             DODOMA

                                    TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI06.06.2012

YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

Ndg. Waandishi wa HabariMwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadalaambavyo vilikuwa:
1. Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%
2. Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei
3. Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).
4. Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopoya elimu ya juu.
Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli iliyowasilishwa Bungeni naKambi ya Upinzani.Mapendekezo mawili,
(1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
(2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa lakiniSerikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.
Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadiyake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa.Halikadhalika Kambi ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao(sitting allowances).
Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahirikwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezajekutekeleza Bajeti ya 15trillioni?

Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo nakuishinikiza Serikali kuyatekeleza.
1.Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa. Hivi sasamisamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% yaPato la Taifa.
2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.
3. Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.
4.Kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto yamikopo kwa wanafunzi.
5.Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa haliya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.
6.Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndaniyanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidikwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi.
7.Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.
8.Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wabei.
9.Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa elimu kwa ubora zaidi,ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory authority)
10.Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchnihasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.
Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa deni la Taifa amabalolimefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasakwenye magari na posho mbalimbali na Kwamba fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa yamaendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango waMaendeleo wa Miaka mitano Asanteni sana!…………………………….

Zuberi Kabwe Zitto(Mb)
Waziri Kivulu-Fedha na Uchumi.

No comments: