Kamanda Butusyo ametaja majina ya marehemu hao kuwa ni pamoja na Immanuel Mwanjanja Mkazi wa Ilomba na Uyole,Mwaniwe Focus,Mkazi wa Chunya na Uyole,Lucia Livingstone(51),Mkazi wa Katumba,wilayani Rungwe,Lena Ngomano(49),Mkazi wa Ngumbulu Isongole,mkazi wa Rungwe,Pius Mbeya,mkazi wa Uyole,Mwase Pius,Mkazi wa Iganzo,jijini Mbeya.
Wengine ni pamoja na Bahati Jafari (33),Mkazi wa Kyela,Ernesta kikanga (62),Mkazi wa Ifunda Iringa,Mwasa Diamond(40),Dereva wa Costa Mkazi wa Ilomba CCM,jijini hapa na Yerusalemu Mwakyusa (35),Mkazi wa jijini Mbeya.
Kamanda Butusyo amewataja majeruhi saba wanaoendelea na matibabu ni Zainabu Bahati(33),Mkazi wa Igawilo,Catherine Komba(23),Mkazi wa Hatwelo,Neema Mwakalukwa,Mkazi wa Mlowo,Veronika Charles (57),Mkazi wa Iringa,Paulina Francis (41),Mkazi wa Uyole,Esther Mgaya (21),Mkazi wa Ujuni na Ford Mwakabungu(35),Mkazi wa Kyela.
Hata hivyo Kamanda huyo amesema dereva na msaidizi wake haijafahamika walipo baada ya tukio na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa mfumo wa breki na hatimaye trela la Lori kuligonga basi na kupinduka baada ya kumshinda.
No comments:
Post a Comment