Thursday, June 14, 2012

MSIMAMO WA WAISLAMU JUU YA SENSA 2012, HUU HAPA

 Kutoka kulia ni Shabani Simba - Afisa Habari na Uhusiano BAKWATA makao Makuu, Sheikh Musa Kundecha Amir wa Baraza kuu la Jumiya na Taasisi za Kiislam Tanzania (BARAZA KUU) pale alikuwa akitoa tamko kama kaimu Mwenyekiti wa jopo la Viongozi wa jumuiya na taasisi zilizo hudhuria mkutano wa sensa Mjini Dodoma, Kondo Bungo Amir wa Jumuiya ya Wahadhiri Tanzania, Ustaadhi Omar Msinziya- Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Makao Makuu, Sadiki Suleiman - Mkurugenzi Mtendaji Jumuiya Wataalam Waislam Tanzania (TAMPRO)
Msimamo wa Waislam juu ya Sensa ya August 2012
1.Kipengele cha dini kiwepo ili kuondoa utata uliopo sasa kwa kupata taarifa rasmi za kiserikali kuliko kuacha kila mtu atoe za kwake, hali hii inaweza kuchochea kuvunjika kwa amani
2. Iundwe tume huru kusimamia zoezi la kuhesabu watu ili kila kundi liridhike
3. Serikali itunge sheria na kuisimamia kupiga marufuku utoji takwimu holela hasa katika shughulirasmi na za serikali jambo ambalo linaweza kuleta uvunjifu wa amani na utulivu kama walivyofanya TBC1 kwa kurusha taarifa zisizorasmi za sensa.Kuendelea kupuuza malalamiko haya ni kukaribisha hisia za dharau, na kutosikilizwa kwa waislam ambako knaweza kuleta shida siku za usoni.
Tamko hili limesomwa  na Sheikh Musa Kundecha kwa niaba ya Sheikh Mohamed Mtuliya (BAKWATA) ambaye ni Mwenyekiti wa Viongozi waliotoa Tamko.Viongozi hao ni wawakilishi wa Taasisi kubwa za kiislam zifuatazo;

1. BAKWATA 2. BARAZA KUU 3. SHIA ITHNAASHERI 4. JOPO LA MAULAMAA TANZANIA 5. HAIYATUL ULAMAA 6. JUMUIYA YA BOHORA 7. UMOJA WA WAHADHIRI TANZANIA 8. JUMUIYA YA WATAALAM WAISLAM TANZANIA 9. SUNNI JAMAAT 10.JUMUIYA YA ISMAILIYA TANZANIA


Imenukuliwa kutoka Michuzi blog

No comments: