Sunday, June 10, 2012

MPYA KABISAAAA ----- SAITOTI WA KENYA AFARIKI


Waziri wa Usalama wa ndani Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea leo asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong takriban kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Abiria wote saba waliokuwa kwenye helikopta hiyo wamefariki dunia na miili yao kuteketezwa kwa kiasi cha kutoweza kutambulika.

Bwana Saitoti na maafisa wengine wa juu katika wizara ya usalama wa ndani walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa mkutano wa usalama. Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema waliona helikota hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa NgongNo comments: