Thursday, May 17, 2012

MAFISANGO KUAGWA KESHO

Kwa mujibu wa meneja wa Simba Nico Nyagawa - Mwili wa Mafisango baada ya kuagwa utaondoka na kusafirishwa na ndege ya shirika la KQ kuelekea kwao Rwanda kwa ajili ya mazishi.

Nyagawa amewaomba wapenzi wote wa Simba na soka kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumuaga kipenzi chao, mchezaji ambaye enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa katika kuisadia Simba kupata mafanikio waliyoyapata msimu huu.
Mafisango aliyekuja nchini mwaka juzi na kujiunga na Azam kabla ya kuhamia Simba mwaka jana, alizaliwa Machi 7, mwaka 1987 mjini Kinshasa, DRC alikoanzia soka kabla ya kuhamia Rwanda, ambako baadaye alichukua uraia wa nchi hiyo.
Kabla ya kuja Tanzania alichezea APR ya Rwanda. Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea Simba ilikuwa dhidi ya Al Ahly Shandy nchini Sudan Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.

Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo Simba katika safu ya kiungo na jana tu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nange 'Kaburu' alisema kiungo huyo yupo kwenye mpango wa kocha wa kikosi cha msimu ujao.

Pamoja na kucheza kama kiungo, Mafisango pia anamudu kucheza nafasi ya beki wa kushoto na beki wa kati.

Japokuwa alikuwa kiungo, lakini pia alikuwa hodari wa kufunga mabao na msimu huu imeshuhudiwa akiifungia Simba mabao 11 katika Ligi Kuu na manne kwenye Kombe la Shirikisho.

No comments: