Wednesday, May 23, 2012

HII NDO TAFAKARI YA TUZO BAADA YA FAWASCO- SAUT MWANZA KUMALIZIKA WADAU WANASEMA NINI..

UTATA WA GOLI KIPA

ERICK …. Jamaa huyu ndie aliepewa tuzo ya kuwa kipa bora wa mashindano, katika michezo 3 aliyocheza amefungwa goli 2 , katika michezo hiyo alimaliza dakika 90 michezo miwili na mmoja alicheza nusu ya pili. Idadi ya mechi alizocheza amezithibitisha kwa njia ya simu.

ABUU JUMAA ……. Kama goili kipa bora alifungwa goli mbili , lakini amecheza mechi nyingi kuliko huyo aliekuwa golikipa bora… yeye huyu amecheza mechi 7 za mashindano, na alimaliza dakika zote za michezo aliyecheza, tofauti na Erick ambae pia ni kipa wa TOTO AFRICA.

UTATA BEKI BORA NA MCHEZAJI BORA


BEKI BORA …… NICKSON KAYOMBO (BAED II) kwa mujibu wa wafuatiliaji wa mambo ya soka katika mashindano ya FAWASCO jamaa huyu nacheza namba 6 uwanjani. Kwa mujibu wa wao pengine angekuwa mchezaji bora na sio beki bora.

MCHEZAJI BORA …….. MESHACK GEORGE (MASS COM), huyu alinyakua zawadi ya mchezaji bora, jamaa huyu anacheza nafasi ya ulinzi “mkoba” kiuhalisia huyu ni beki …. Kama hoja ni beki bora , kwa kuwa mchezaji bora ni BEKI basi hapakuwa na haja ya kuwa na beki bora kutoka nafasi nyingne, kama beki ndio mchezaji bora.

HATA HIVYO ...tunatoa pongezi kwa timu zote na waandaaji wa michuano hii ... moja ya ligi zenye donge nono hapa nchini...
PICHA ZOTE NA eliamigongo.blogspot.com

No comments: