Thursday, May 31, 2012

HAYA NI MAAJABU AMBAYO HAYAJAWAHI KUREKODIWA PENGINE... MBUZI WAOPANDA JUU YA MITI KUTAFUTA CHAKULA


Maelezo yanasema, aina hii ya mbuzi inapatikana zaidi nchini Morocco hasa katika maeneo ya Marrakesh na Essaouira.
Mbuzi hawa wamelazimika kukwea mitini ili kutafuta chakula hasa nyakati za kiangazi kigumu ambapo majani ya chini huwa adimu. Vile vile hii ni njia mojawapo ya mbuzi kupunga upepo kutokana na hali ya ukanda wa jangwa katika maeneo hayo. Na sababu nyingine iliyotajwa, ni kuwa hii ni nja ya kujijifadhi, kama lindo, ili kujiepusha na hatari za ardhini.

Lakini pengine sababu mahsusi na ya kipekee ya mbuzi wa Morocco kukwea mtini, inatoka na mti mmoja muhimu sana, unafanana na mzabibu, mbuzi hawa wanatajwa kuyapenda sana matunda ya mti huo.

Picture

Picture

Picture

Picture

Source: http://www.wavuti.com/index.html##ixzz1wTgL4sVF

No comments: